Ripoti: UK, Saudia zaukingia kifua utawala wa Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1651-ripoti_uk_saudia_zaukingia_kifua_utawala_wa_bahrain
Ripoti ya hivi karibuni imefichua kuwa, Saudi Arabia na Uingereza zilishirikiana kuvuruga azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya Bahrain.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 21, 2016 04:32 UTC
  • Ripoti: UK, Saudia zaukingia kifua utawala wa Bahrain

Ripoti ya hivi karibuni imefichua kuwa, Saudi Arabia na Uingereza zilishirikiana kuvuruga azimio la Umoja wa Mataifa dhidi ya Bahrain.

Gazeti mashuhuri la 'The Observer' la nchini Uingereza limefichua habari hiyo na kusema kuwa serikali za Riyadh na London zilifanya juu chini kuhakikisha vipengee muhimu vya azimio la UN dhidi ya rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Bahrain vinaondolewa. Uingereza ilikuwa mstari wa mbele kushawishi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wasipitishe azimio lenye maneno makali ya kukemea na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu huko Bahrain. Gazeti hilo limepata rasimu ya asili ya azimio la Umoja wa Mataifa na taarifa ya mwisho ya umoja huo kuhusu kadhia hiyo ambapo nyaraka mbili hizo zinatofautiana pakubwa. taarifa ya mwisho iliyopitishwa mwaka uliopita kuhusiana na hali ya haki za binadamu nchini Bahrain imepunguzwa makali kinyume na ilivyokuwa rasimu asili. Uingereza ni muuzaji mkubwa wa silaha kwa Saudi Arabia na Bahrain na Saudi Arabia ni muungaji mkono mkubwa wa jinai zinazofanywa na ukoo wa Aal Khalifa dhidi ya wananchi wa Bahrain.