Israel yafanya njama za kuendeleza mzingiro wa kidhulma Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i16546-israel_yafanya_njama_za_kuendeleza_mzingiro_wa_kidhulma_ukanda_wa_gaza
Utawala wa Kizayuni wa Israel unajiandaa kuishambulia meli ya al Zaituna na vile vile kuwazua wanaharakati wa kimataifa kuwasili huko Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Oct 03, 2016 00:29 UTC
  • Israel yafanya njama za kuendeleza mzingiro wa kidhulma Ukanda wa Gaza

Utawala wa Kizayuni wa Israel unajiandaa kuishambulia meli ya al Zaituna na vile vile kuwazua wanaharakati wa kimataifa kuwasili huko Ukanda wa Gaza.

Gazeti la Kizayuni la Maariv limeripoti kuwa wanajeshi wa majini wa Israel wametakiwa kujiweka tayari ili kuwauzia wanaharakati wa kimataifa wa nchi za nje wanaosafiri ndani ya meli hiyo kuwasili huko Ghaza kwa lengo la kuondoa mzingiro wa kidhulma uliowekwa na Israel kwa miaka kadhaa sasa katika eneo hilo. Utawala wa Kizayuni umewaagiza wanajeshi wake hao wa majini kujiweka tayari ikiwa ni katika juhudi za utawala huo za kuikwamisha meli ya al  Zaituna kuwasili huko Gaza. 

Wanaharati wa nchi ajinabi wanaotaka kuondolewa mzingiro Ukanda wa Ghaza

Gazeti la Maariv la Israel limeongeza kuwa, wanajeshi wa majini wa utawaka huo wamepanga kwanza kuisimaisha meli ya al Zaituna na kisha kuipelekea hadi katika bandari ya Asdud na baada ya hapo utawala huo uwarejeshe katika nchi zao wanaharakti hao wa kimataifa. Meli ya al Zaituna hivi sasa inaelekea Ukanda wa Ghaza ikiwa safarini katika siku ya tano ili kuondoa mzingiro wa baharini katika eneo hilo. Meli hiyo inatazamiwa kuwasili Ghaza siku mbili zijazo.