AI: Muungano wa kijeshi unaoongozwa na US umeua raia 300 Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18241-ai_muungano_wa_kijeshi_unaoongozwa_na_us_umeua_raia_300_syria
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetangaza kuwa raia wapatao 300 wa Syria wameuliwa katika mashambulio 11 ya anga yaliyofanywa na Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 27, 2016 10:24 UTC
  • AI: Muungano wa kijeshi unaoongozwa na US umeua raia 300 Syria

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetangaza kuwa raia wapatao 300 wa Syria wameuliwa katika mashambulio 11 ya anga yaliyofanywa na Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani.

Katika ripoti yake liliyotoa hapo jana, Amnesty limeeleza kuwa kamandi kuu ya kijeshi ya Marekani inayoongoza mashambulio ya muungano wa kijeshi ndani ya ardhi ya Syria huenda imefanya "mashambulio yaliyo kinyume cha sheria" katika nchi hiyo ya Kiarabu iliyoharibiwa na vita.

Shirika la Msamaha Duniani limeashiria uzembe uliofanywa na Washington wa kutoepusha kutokea mauaji ya raia katika mashambulio yake nchini Syria na kuongeza kwamba idadi ya raia waliouawa tangu zilipoanza operesheni za muungano wa kijeshi nchini Syria yamkini ikawa watu wapatao 600 au zaidi.

Ndege za Marekani zikielekea Syria kufanya mashambulio 

Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limetoa vielelezo kadhaa vya kuthibitisha na kutilia nguvu ripoti yake zikiwemo filamu za video, picha za satalaiti, maelezo ya mashuhuda pamoja na ripoti za vyombo vya habari na makundi ya haki za binadamu na kuchunguza mashambulio 11 yaliyofanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani, ambao umeingia katika anga ya Syria bila ya idhini ya serikali ya Damascus kwa kisingizio cha kushambulia ngome za makundi ya kigaidi…/