Amnesty International: Mauaji ya kimbari yanafanyika Gaza
Agnes Calamard Mkuu wa Shirika la Amnsety International Jumamosi usiku alirusha puto la hewa moto katika anga ya Paris ambalo juu yake aliandika maneno yanayosomeka: "Mauaji ya kimbari yanaendelea huko Gaza. Sitisha mauaji hayo."
Televisheni ya al Jaeera ya Qatar imeripoti kuwa: Puto hilo limebeba mwenge usio wa Olimpiki kwa Michezo ya Paris 2024 katika maadhimisho ya kwanza ya michezo hiyo.
Calamard ameandika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba: Shirika la Amnesty International limeikumbusha Ufaransa kwamba mauaji ya kimbari yanajiri katika Ukanda wa Gaza, na maneno au ahadi za viongozi wa Ufaransa hazitoshi.
Bi Calamard ameongeza kuwa: Tunapasa kuchukua hatua za haraka na chanya ili kuhitimisha njaa iliyosababishwa na Israel. Tunapasa kuchukua hatua ili kukomesha mauaji ya kimbari huko Gaza na tuchukue hatua tuhitimishe kinga ya Israel.
Katika kipindi cha vita vya kichokozi vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza Oktoba 7, 2023 na kuendelea hadi sasa; utawala huo unaendelea kufanya jinai za kimfumo dhidi ya wananchi wa Palestina. Moja ya vipengele vya wazi zaidi vya jinai hizo ni mashambulizi ya makusudi dhidi ya makazi, shule, hospitali, kambi za wakimbizi, na hivi karibuni kumeshuhudiwa mashambulizi katika vituo vya kusambaza misaada ya kibinadamu chini ya usimamizi wa Marekani na utawala ghasibu wa Israel.
Katika miezi ya karibuni, utawala wa Kizayuni umekuwa ukitumia utaratibu wa usambazaji misaada ya kibinadamu uliobuniwa na Marekani kwa ushirikiano na Tel Aviv ambapo Israel iliwaelekeza Wapalestina wanaohitaji misaada katika maeneo maalumu huko Gaza na kisha kuwashambulia kwa makombora na mabomu wakati wa kupokea misaada hiyo.