Mjumbe wa UN atadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i19066-mjumbe_wa_un_atadharisha_kuhusu_hali_mbaya_ya_kibinadamu_inayoikabili_yemen
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2016 12:07 UTC
  • Mjumbe wa UN atadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili Yemen

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen ametahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayoikabili nchi hiyo.

Ismail Ould Sheikh Ahmed, amesema leo kuwa hali ya Yemen ni mbaya mno na hakuna taasisi yoyote ya kimataifa inayojali kuhusu mauaji ya raia wa Yemen.

Huku akiashiria kuwa uchumi wa Yemen unakaribia kuporomoka kikamilifu, Sheikh Ahmed amegusia pia mkutano wake na viongozi wa mirengo ya kisiasa ya nchi hiyo na kueleza kwamba katika mazungumzo na ujumbe wa Ansarullah na wa chama cha Kongresi ya Wananchi wamebadilishana mawazo juu ya masuala mengi lakini pande mbili hizo zingali kila moja inashikilia msimamo wake wa awali juu ya baadhi ya masuala.

Ismail Ould Sheikh Ahmed, mjumbe wa UN Yemen

Mjumbe huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen amezitaka pande zote nchini humo zilegeze misimamo yao kwa ajili ya wananchi na ili kuweza kufikia amani kamili na itakayojumuisha pande zote.

Hali mbaya ya uhaba wa chakula pia inaikabili Yemen

Juhudi za Umoja wa Mataifa za kufanikisha utekelezaji wa usitishaji vita na kuanzisha tena mazungmzo ya amani ya Yemen hadi sasa zimeshindwa kuzaa matunda na hii ni katika hali ambayo kimya cha taasisi hiyo kuu ya kimataifa mbele mauaji ya raia wa Yemen yanayofanywa na utawala vamizi wa Saudia umeufanya Umoja wa Mataifa uonekane mshirika wa jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saud dhidi ya wananchi madhulumu na wasio na hatia wa Yemen.../