Bahrain yalaaniwa kwa kuanzisha uhusiano na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i22345-bahrain_yalaaniwa_kwa_kuanzisha_uhusiano_na_israel
Utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain umelaaniwa vikali kwa hatua yake ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 29, 2016 03:53 UTC
  • Bahrain yalaaniwa kwa kuanzisha uhusiano na Israel

Utawala wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain umelaaniwa vikali kwa hatua yake ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.

Zaidi ya wanaharakati 400 wa haki za binadamu nchini Bahrain wamelaani hatua ya Idara ya Biashara ya Utawala wa Aali Khalifa kushirikiana na Makuhani wenye misimamo ya kufurutu ada pamoja na Wazayuni kadhaa katika kuandaa sherehe ya Kizayuni ya Hanukkah katika mji mkuu wa nchi hiyo, Manama.

Katika taarifa, wanaharakati hao wametaka wafanyabiashara wote Wabahrain walioshiriki katika sherehe hiyo ya Kizayuni kuadhibiwa. Huku wakilaani kufanyika sherehe hiyo  ya Kizayuni mjini Manama, wametangaza kufungamana kwao na mapambano ya Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza udharura wa kuundwa taifa huru la Palestina mji wake mkuu ukiwa ni Quds Tukufu.

Makuhani walioshiriki katika shehrehe hioyo mjini Manama Jumamosi wanaamini kuwa Wapalestina wanapaswa kuangamizwa kwa umati. Ujumbe wa makuhani hao ulifika Bahrain kwa mwaliko rasmi wa mfalme wa nchi hiyo Hammad bin Issa Aal Khalifa.

Wazayuni wenye misimamo ya kuwaangamiza kwa umati Wapalestina wakiwa na wafanyabiashara wa Bahrain mjini Manama

Wakati huo huo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, imelaani vikali hatua ya ufalme wa Bahrain kuwa mwenyeji wa makuhani hao wa Kizayuni wenye misimamo mikali.

Taariifa ya Hamas imesema ni jambo la aibu na udhalilishaji mkubwa kuona watawala na wafanyabiashara wa Bahrain wakiwakaribisha na wakicheza densi  na ujumbe wa Mayahudi na Wazayuni wabaguzi na wenye misimamo mikali

Tokea mwaka 2011, wananchi wa Bahrain walianzisha mwamako wa Kiislamu kwa lengo la kupinga utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa na wamekuwa wakiendeleza maandamano ya amani karibu kila siku tokea wakati huo.