Israel yaendeleza ukatili wake, yaua shahidi Wapalestina 2
(last modified Thu, 24 Mar 2016 15:06:25 GMT )
Mar 24, 2016 15:06 UTC
  • Wapalestina wauliwa shahidi
    Wapalestina wauliwa shahidi

Askari wa utawala wa kizayuni wa Israel wameua shahidi Wapestina wawili kwa kuwafyatulia risasi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Jeshi katili la Israel limedai kuwa limetekeleza unyama huo eti baada ya vijana hao kushambulia askari wake kwa visu katika mji wa al-Khalil. Mji huo ambao ndio mkubwa zaidi katika Ukingo wa Magharibi, umekuwa ukishuhudia makabiliano kati ya Wapalestina wapatao laki 2 na walowezi wa kizayuni ambao wanaishi chini ya ulinzi mkali wa askari wa utawala huo haramu.

Alkhamisi iliyopita, jeshi katili la utawala wa kizayuni wa Israel liliua shahidi vijana wawili wa Kipalestina, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Zaidi ya Wapalestina 200 wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameuawa shahidi na jeshi la utawala ghasibu wa Israel tangu Oktoba mwaka jana, baada ya kuanza Intifadha ya 3 ya kuzikomboa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.