Answarullah: Wasaudia na Marekani watazame upya mahesabu yao kuhusu Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i42432-answarullah_wasaudia_na_marekani_watazame_upya_mahesabu_yao_kuhusu_yemen
Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen, Mohammed Ali al-Houthi amegusia nguvu za muqawama wa wananchi wa Yemen dhidi ya jinai za wavamizi na kumtaka Mohammad Bin Salman na nchi washiriki katika muungano vamizi pamoja na Marekani, kuangalia upya mahesabu yao kuhusu nchi hiyo ya Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 30, 2018 23:54 UTC
  • Jeshi la Yemen liko imara kuihami nchi mbele ya uvamizi wa Saudia
    Jeshi la Yemen liko imara kuihami nchi mbele ya uvamizi wa Saudia

Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen, Mohammed Ali al-Houthi amegusia nguvu za muqawama wa wananchi wa Yemen dhidi ya jinai za wavamizi na kumtaka Mohammad Bin Salman na nchi washiriki katika muungano vamizi pamoja na Marekani, kuangalia upya mahesabu yao kuhusu nchi hiyo ya Kiarabu.

Al-Houthi ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya al-Mayadeen ya nchini Lebanon na kuongeza kuwa, viongozi wa Yemen walioko upande wa Saudia hadi sasa wanashikiliwa mjini Riyadh na utawala wa Aal-Saud na hawawezi hata kutoa maoni yoyote kuhusiana na kile kinachoendelea nchini kwao Yemen.

Mohammed Ali al-Houthi, Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen

Aidha Mkuu wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen amezungumzia kuanza maandalizi ya duru mpya ya mazungumzo ya amani kuhusu Yemen na kusema, mazungumzo yoyote lazima yawe chanya na yasiwe kama mazungumzo yaliyopita ambapo Mjumbe maalumu wa zamani wa Umoja wa Mataifa hakuzingatia misingi ya kutopendelea upande mmoja. Kadhalika Mohammed Ali al-Houthi amesema kuwa, ni lazima uingiliaji wa Marekani na uungaji mkono wa kifedha wa Wasaudia kwa pande zinazoshiriki katika mazungumzo hayo na kwa lengo la kuzirubuni, ukomeshwe.

Martin Griffiths, mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen

Alkhamisi iliyopita, Mkuu huyo wa Baraza Kuu la Mapinduzi nchini Yemen alikutana mjini Sana'a na Martin Griffiths, mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen na kuzungumza naye juu ya mwenendo wa mazungumzo ya amani, ambapo alisema kuwa, mashambulizi ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen yametoka nje ya udiplomasia na hata sheria za kimataifa.