Jun 21, 2018 13:54 UTC
  • Mke wa Netanyahu afunguliwa kesi ya ufisadi wa kifedha

Mke wa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amefunguliwa rasmi faili la kesi ya ufisadi wa kifedha.

Wizara ya Sheria ya Israel imesema leo Alkhamisi kuwa, Sara Netanyahu anatuhumiwa kufuja fedha za umma zaidi ya dola laki moja kuagiza vyakula vya kifahari licha ya makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa utawala huo haramu kuwa na wapishi wa kutosha.

Haijabinika kesi dhidi yake itaanza kusikilizwa lini, lakini iwapo atapatikana na hatia atahukumiwa kifungo cha hadi miaka mitano jela.

Mke wa Netanyahu amekuwa akiishi maisha ya kifahari na kudhalilisha watu wa tabaka la chini. Mwaka 2016 aliagizwa na mahakama kumpa mfanyakazi wake dola 42,000 za Marekani, baada ya kupatikana na hatia ya kumdhulumu na kumdhalilisha.

Tangu ulipoanzishwa utawala haramu wa Israel viongozi kadhaa wa utawala huo pandikizi wamewekwa jela kutokana na ufisadi wa aina mbalimbali ukiwemo ufisadi wa kifedha.

Sara Netanyahu

Benjamin Netanyahu, Ehud Barak, Ariel Sharon na Ehud Olmert, ni miongoni mwa mawaziri wakuu wa Israel ambao wamewahi kusailiwa na polisi ya utawala huo bandia kutokana na ufisadi wa kifedha. 

Karibu kila wiki Waisraeli wamekuwa wakifanya maandamano kwa lengo la kumshinikiza Netanyahu ambaye anaandamwa na kashfa nyingi za ufisadi wa kifedha ang’atuke madarakani.

Tags