Apr 25, 2019 13:46 UTC
  • Dunia yaendelea kulaani jinai mpya za utawala wa Saudi Arabia

Mashirika na taasisi za kimataifa pamoja na wanaharakati wa masuala ya kijamii wanaendelea kulaani jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Aal Saud wa Saudi Arabia ya kuwaua kwa umati raia 37 wa nchi hiyo.

Baadhi ya wanaharakati hao jana walikusanyika mbele ya ubalozi wa Saudia mjini London Uingereza wakipiga nara za mauti wa ukoo wa Aal Saud.

Katika harakati hiyo ya kulaani jinai za Saudia, wanaharakati hao walibeba picha za watu waliouliwa kwa umati huko Saudi Arabia zikiwa zimeandikwa: "Wasusieni wauaji kama hawa" na "kuiunga mkono Saudia ni sawa na kuunga mkono jinai."

Wanaharakati hao wamelaani pia kimya cha tawala za nchi za Magharibi mbele ya uvunjaji huo mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Aal Saud na kuzitaka nchi hizo ziache kuisaidia Saudia katika jinai zake hizo.

Saudia.. ardhi ya ukatili wa umwagaji damu

 

Taasisi mbalimbali za kimataifa nazo zimeendelea kulaani jinai hiyo ya kuuliwa kwa umati raia 37 wa Saudi Arabia na hasa njia iliyotumiwa kufanya mauaji hayo. Taarifa zinasema kuwa maafisa wa Saudi Arabia wamewaua raia hao 37 wa nchi hiyo kwa kuwakata vichwa.

Umoja wa Ulaya umetoa taarifa na kulaani jinai hiyo ingawa kulaani tu hakusaidii kitu madhali nchi za Ulaya zinaendelea kuwaunga mkono kwa hali zote watawala wa Saudi Arabia.

Katika Umoja wa Mataifa pia Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa umoja huo amelaani jinai hiyo mpya ya Saudi Arabia.

Tags