Saudi Arabia yatakiwa ikomeshe uadui wake dhidi ya taifa la Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i55175-saudi_arabia_yatakiwa_ikomeshe_uadui_wake_dhidi_ya_taifa_la_yemen
Yahya Ali al-Qahoum, afisa Mwandamizi wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameitaka Saudi Arabia ikomeshe uadui wake dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 04, 2019 03:35 UTC
  • Saudi Arabia yatakiwa ikomeshe uadui wake dhidi ya taifa la Yemen

Yahya Ali al-Qahoum, afisa Mwandamizi wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameitaka Saudi Arabia ikomeshe uadui wake dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Yemen.

Kanali ya Televisheni ya al-Mayadeen imemnukuu mjumbe huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen akikosoa vikali siasa za kivamizi za muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen na kueleza kwamba, watawala wa Riyadh wanapaswa kuangalia upya mahesabu yao hasa baada ya kupata hasara kubwa na kushindwa kufikia malengo yao katika vita huko Yemen.

Wakati huo huo, mtandao wa habari wa Middle East Monitor umeashiria hatua ya Imarati ya kutangaza kuondoka katika vita nchini Yemen na kubainisha kwamba, kwa hatua yake hiyo Abu Dhabi imejiokoa na madhila ya kushindwa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia.

Mashambulio ya Saudi Arabia yanavyoibomoa nchi masikini ya Yemen

Mtandao huo wa habari unaendelea kueleza kwamba, baada ya Imarati kujiondoa huko Yemen, sasa Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia utaubeba peke yake mzigo wa aibu na madhila ya kushindwa katika vita huko Yemen.

Wayemeni zaidi ya elfu kumi na sita wameuawa hadi sasa, makumi ya maelfu kujeruhiwa na mamilioni ya wengine wamekuwa wakimbizi tangu Saudi Arabia na waitifaki wake Imarati, Marekani na nchi nyingine kadhaa zilipoanzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu mwezi Machi mwaka 2015 na kuiwekea mzingiro wa baharini, nchi kavu na anga.