Syria yapinga kuundwa kinachodiwa 'eneo salama' kaskazini mwa nchi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56692-syria_yapinga_kuundwa_kinachodiwa_'eneo_salama'_kaskazini_mwa_nchi
Syria imelaani jitihada za Uturuki za kunda eneo inalodai kuwa eti ni salama kaskazini mwa nchi hiyo na kuitaka Ankara iache kuingilia mambo yake ya ndani.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Oct 18, 2019 03:53 UTC
  • Syria yapinga kuundwa kinachodiwa 'eneo salama' kaskazini mwa nchi

Syria imelaani jitihada za Uturuki za kunda eneo inalodai kuwa eti ni salama kaskazini mwa nchi hiyo na kuitaka Ankara iache kuingilia mambo yake ya ndani.

Buthaina Shaaban, mshauri wa kisiasa wa Rais wa Syria, akizungumza Alhamisi, usiku ameashiria namna ambavyo jamii ya kimataifa inapinga uvamizi wa Uturuki dhidi ya eneo la kaskazni mwa Syria kwa kisingizio cha kupambana na wanamgambo wa Kikurdi na kuunda eneo eti salama ndani ya ardhi ya Syria na kusema: "Ili uthabiti upatikane katika eneo,  askari wa Uturuki wanapaswa kuondoka mara moja katika ardhi ya Syria." Aidha amesema hatua ya Uturuki kuunda eneo  'salama' kaskazini mwa Syria lazima isitishwe mara moja.

Bi. Shaaban amesema hatua ya Uturuki kukubali usitishwaji vita haraka kaskazini mwa Syria inatokana na upinzani mkubwa wa jamii ya kimataifa kwa uvamizi wake katika maeneo hayo ya  Wakurdi. Hali kdhalika amesema sababu nyingine ambayo imeifanya Uturuki kukubali usitishwaji vita ni mapambano ya wananchi, jeshi na wapiganaji wa Kikurdi kaskazini mwa Syria.

Rais Erdogan wa Uturuki na Makamu wa Rais wa Marekani Pence mjini Ankara 17 Oktoba 2019

Wiki moja baada ya Uturuki kuvamia eneo la kaskazini mwa Syria, siku ya Alhamisi Marekani na Uturuki ziliafikiana kuhusu usitishwaji vita wa siku tano katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mapatano hayo, wanajeshi wa Uturuki watasitisha oparesheni zao za kijeshi kaskazini mwa Syria kwa muda wa siku tano iili kuwapa fursa wanamgambo wa Kikurdi warudi nyuma umbali wa maili 20 ndani ya ardhi ya Syria kutoka mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.

Wiki iliyopita Uturuki ilianzisha hujuma dhidi ya Syria ambapo Rais Erdogan amesema lengo la mashambulizi hayo ni kuangamiza kundi la PKK la eneo la Kurdistan la Uturuki na pia kundi la Wakurdi wa Syria linalojulikana kama PKK. Uturuki imetekeleza shambulizi lake dhidi ya Syria pamoja na kuwa oparesheni hiyo imepingwa vikali kieneo na kimataifa. Baadhi ya duru zinadokeza kuwa hadi sasa watu 270 wameuawa katika opareshni hiyo huku makumi ya maelfu wakiwa wakimbizi.