Wairaq wataka kufungwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i58252-wairaq_wataka_kufungwa_ubalozi_wa_marekani_mjini_baghdad
Makundi mbalimbali ya wananchi nchini Iraq yameendelea kutoa wito na kushinikiza kufungwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 01, 2020 21:44 UTC
  • Wairaq wataka kufungwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad

Makundi mbalimbali ya wananchi nchini Iraq yameendelea kutoa wito na kushinikiza kufungwa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.

Jawad al-Talibawi, mmoja wa makamanda wa Harakati ya Wananchi ya al-Hashd al-Sha'abi amesema kuwa, ubalozi wa Marekani mjini Baghdad unapaswa kufungwa kwani ni pango la ujasusi na mahali pa kupangia njama za uharibifu dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu.

Aidha amesema kuwa, matukio yanayotokea mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad ni radiamali ya kawaida dhidi ya mashambulio ya anga ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya wapiganaji wa al-Hashd al-Sha'bi.

Wakati huo huo, Muhammad Muhyi, msemaji wa Brigedia ya Hizbullah, tawi la kijeshi la Hashd al-Sha'abi amesisitiza juu ya kudumishwa mkusanyiko wa wananchi mbele ya ubalozi wa Mareakni mjini Baghdad hadi ubalozi huuo utakapofungwa.

Matukio ya picha mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Baghdad

Katika upande mwingine, miito mbalimbali imeendelea kutolewa inayolitaka Bunge na serikali ya Iraq kupasisha haraka sheria ya kutimuliwa nchini humo wanajeshi wa Marekani pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wao mjini Baghdad.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, waandamaji wa Kiiraq wanaondamana na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekkani mjini Baghdad wameweka mahema wakijiandaa kufanya mkusanyiko mwingine mkubwa mbele ya ubalozi huo.

Itakumbukwa kuwa, hasira za wananchi wa Iraq zinatokana na hatua ya Marekani ya kushambulia vituo viwili vya Al Hashd al Shaabi katika mji wa Al Qaim katika mpaka wa Iraq na Syria ambapo katika hujuma hiyo wanachama 25 wa Al Hashd al Shaabi waliuawa shahidi na wengine 51 kujeruhiwa.