Martin Griffiths ataka kusitishwa vita mara moja nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i59601-martin_griffiths_ataka_kusitishwa_vita_mara_moja_nchini_yemen
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masala ya Yemen ametoa wito wa kusitishwa vita mara moja na bila ya masharti yoyote nchini Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2020 11:56 UTC
  • Martin Griffiths ataka kusitishwa vita mara moja nchini Yemen

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masala ya Yemen ametoa wito wa kusitishwa vita mara moja na bila ya masharti yoyote nchini Yemen.

Martin Griffiths  ambaye alikuwa safarini katika mkoa wa Maʾrib huko mashariki mwa Yemen amesisitiza udharura wa kuanza mazungumzo ya kisiasa baina ya makundi yote ya Yemen kwa ajili ya kusitisha vita na kudumishwa mazungumzo ya kurejesha amani nchini humo.

Griffiths amesema kuwa, mkoa wa Maʾrib unapaswa kulindwa kama kituo cha wakimbizi na haupaswi kuwa medani ya mapigano na vita. Mjumbe Maalumu wa UN nchini Yemen ametahadharisha kwamba, kuendelea mapigano nchini humo kutaididimiza zaidi Yemen katika shimo la moto wa vita na umaskini.

Saudi Arabia inaendelea kuua raia wasio na hatia wa Yemen

Maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi tangu Saudi Arabia na washirika wake walipoanzisha mashambulizi dhidi ya taifa la Yemen mwezi Machi mwaka 2015.   

Saudi Arabia na washirika wake pia wanazingira Yemen kutokea pande zote na wanazuia kuingizwa nchini humo mahitaji muhimu kama chakula, madawa na kadhalika.