Shambulio dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa, jibu huko Tel Aviv
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i83342-shambulio_dhidi_ya_msikiti_wa_al_aqsa_jibu_huko_tel_aviv
Kufuatia wito uliotolewa na walowezi wenye misimamo mikali ya Kiyahudi wa kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya kumbukumbu ya kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina na kutangazwa dola haramu la Israel, Wapalestina wametekeleza oparesheni nyingine katika kitongoji cha walowezi hao cha El'ad huko Mashariki mwa Tel Aviv. Wazayuni watatu wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
May 07, 2022 03:37 UTC
  • Shambulio dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa, jibu huko Tel Aviv

Kufuatia wito uliotolewa na walowezi wenye misimamo mikali ya Kiyahudi wa kushambuliwa Msikiti wa Al-Aqsa katika siku ya kumbukumbu ya kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina na kutangazwa dola haramu la Israel, Wapalestina wametekeleza oparesheni nyingine katika kitongoji cha walowezi hao cha El'ad huko Mashariki mwa Tel Aviv. Wazayuni watatu wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa.

Hiyo ni operesheni ya tano ya wanamapambano wa Kipalestina katika wiki chache za hivi karibuni. Vijana waliotekeleza operesheni hiyo mpya ni Asad Youssef al-Rifai mwenye umri wa miaka 19 na Sobhi Emad Abu Shaqir mwenye umri wa miaka 20, ambao wote ni kutoka Kaskazini Magharibi mwa Jenin huko Kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi. Kitongoji cha walowezi cha El'ad kina Wayahudi wapatao 150,000 wa dhehebu la Haredim, waliowachache katika dini ya Kiyahudi. Kitongoji hicho kilianzishwa mwaka 1990 katika ardhi iliyoghusubiwa ya Palestina, lakini idadi ya wakazi wake imeongezeka haraka sana.

Operesheni ya El'ad sawa na zilizoitangulia, imefanyika wakati vikosi vya jeshi na usalama vya utawala wa Kizayuni vikiwa katika hali ya tahadhari kutokana na sherehe za kuasisiwa dola haramu la Kizayuni katika ardhi ya Palestina na kutangazwa uwepo wa Israel, na wakati maonyo ya kiusalama yalikuwa bado hayajapungua kutokana na operesheni kadhaa za kujitoa mhanga za hapo awali.

Wazayuni 3 waaangamizwa katika Oparesheni ya Siku ya Nakba huko Elad 

Operesheni hizi sambamba na kuzidisha umoja na mshikamano baina ya Wapalestina, zinazidisha na kupanua mifarakano ya ndani kati ya Wazayuni. Ukitoa Mahmoud Abbas, Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, makundi mengine yote ya Wapalestina yameunga mkono na kupongeza operesheni hiyo; na watu wa Palestina, kama kawaida, wanasherehekea mafanikio hayo; kinyume chake, kwa upande wa Israel hali ni tofauti kabisa. Mazingira ya wasiwasi na vitisho yanatawala jamii ya Wazayuni, na serikali ya muungano ya Bennett-Lapid inaelekea kuporomoka. Makundi hasimu ya kisiasa yanayoongozwa na Benjamin Netanyahu nje ya muungano unaotawala, yanailaumu serikali ya Naftali Bennett kuwa imefanya uzembe, na yanaendelea kuwachochea wanachama wenye itikadi kali wa mrengo wa walowezi yakiwahamasisha kujiondoa katika muungano wa serikali inayotawala huko Tel Aviv. Muhimu zaidi ni kwamba, hali ya kutoaminiwa jeshi na vyombo vya ulinzi na usalama vya Israel imeongezeka, na ushiriki mkubwa wa Wapalestina wanaoishi katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 katika operesheni dhidi ya Uzayuni na pia katika mikusanyiko na maandamano ya kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa, umeibua wasiwasi baina ya Wazayuni. Hii ni kwa sababu, idadi ya Wapalestina hao inazidi milioni mbili na wana fursa ya kusafiri na kuwepo katika eneo lote la Palestina inayokaliwa kwa mabavu na ikibidi wanaweza kutimiza malengo ya Wapalestina walio nje ya ardhi hizo. 

Maafisa wa Kizayuni wa Israel wamembebesha lawama za operesheni hiyo Yahya Sinwar ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na wametoa wito wa kuuawa kwake. Katika hotuba yake kwenye maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwenye Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani, Sinwar alipongeza operesheni za Wapalestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Hata hivyo ukweli ni kwamba, oparesheni hizi zinazofanywa kwa kujitolea na bila ya kuratibiwa na kundi lolote, zilianza kabla ya matamshi hayo ya Yahya al-Sinwar; na operesheni ya El'ad ilikuwa ya tano katika mfululizo huo kwenye mwezi uliopita, ambapo Wazayuni 18 waliuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa. 

Operesheni nyingi za Wapalestina zimejikita zaidi katika maeneo yaliyokaliwa kwa mabavu na Israel mwaka 1948 hususan Tel Aviv, mji mkuu wa kisiasa wa utawala huo ghasibu. Watekelezaji wa operesheni hizo ama ni Wapalestina wanaoishi katika ardhi hizo ambao ni raia wa Israel au wakazi wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kwenye kambi za wakimbizi wa Kipalestina. 

Siku ya Kimataifa ya Quds 

Inaonekana kuwa, operesheni hizo zinaambatana na ujumbe unaotumwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba iwapo utawala huo utaendeleza mipango yake ya kujitanua na kuwapa makazi Wazayuni wenye misimamo mikali katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki, na kuvuruga kabisa matumaini ya kuundwa nchi huru ya Palestina mji wake mkuu ukiwa Quds (Jerusalem), Wapalestina pia watachukua hatua za kukabiliana na mipango hiyo ya Wazayuni. Kwa hakika, sababu ya operesheni hizo kulenga zaidi Tel Aviv ni kwamba walowezi wanaoshambulia Msikiti wa al Aqsa wanaongozwa na kusimamiwa kutoka katika mji mkuu huo wa utawala wa Kizayuni, hivyo utawala huo hauwezi kujivua na kujitoa hatiani katika mashambulizi ya mara kwa mara ya Wazayuni katika Msikiti huo.

Kwa mantiki hiyo mashambulizi ya kujihami ya Wapalestina yataendelea hadi pale kutakapofanyika mabadiliko ya mielekeo na sera za kupenda kujitanua za utawala wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki na vilevile kuhusiana na hujuma za mara kwa mara za walowezi wenye misimamo mikali ya kidini katika Msikiti wa Al-Aqsa.

Mambo kadhaa yamewafanya Wapalestina wachukue msimamo huo. Kwanza ni kwamba, Wapalestina wamefikia hitimisho kwamba, mbinu yao ya kuwa katika hali ya kujibu mashambulizi imewapa Wazayuni fursa ya kuendelea kukalia kwa mabavu ardhi zaidi katika miongo michache iliyopita. Pili ni kwamba, Wapalestina wameamini kuwa, Israel iliwahadaa wakati wa mazungumzo ya amani na imetumia mazungumzo hayo kupoteza muda ili kutekeleza mipango yake ya upande mmoja na ya kujitanua zaidi. Tatu ni kwamba, tajiriba imedhihirisha kuwa mienendo ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina ilibadilika pale tu walipohisi nguvu ya upande wa pili na kuamini kwamba wakipigana nao watapigwa.

Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana baada ya makundi ya mapambano ya Ukanda wa Gaza yalipoanza kutoa vipigo mtawalia kwa utawala huo wa Kizayuni, Israel haikuthubutu tena kufanya mashambulizi ya anga ya mara kwa mara dhidi ya eneo hilo kama ilivyokuwa hapo awali.