Ripoti: Zaidi ya Wazayuni 200 wakiwemo wanajeshi waliangamizwa mwaka uliopita
Duru za Kizayuni zimetangaza kuwa, zaidi ya Wazayuni 200 waliangamizwa katika mwaka uliopita (2022) katika ardhi za palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.
Kwa mujibu wa duru hizo, miongoni mwa waliouawa katika oepesheni mbalimbali huko Israel wamo wanajeshi 145 wa utawala huo ghasibu.
Idhaa ya jeshi la Israe imenukuu takwimu za Wizara ya Vita ya utawala huo vamizi na kutangaza kuwa, makumi ya wanajeshi wa Israel waliuawa mwaka jana katika operesheni mbalimbali za kijeshi.
Aidha kituo hicho cha Radio cha jeshi kimetangaza kuwa, mwaka uliopita pia zaidi ya majeruhi 86 wa vita walipoteza maisha yao kutokana na athari mbaya za majeruhi na hivyo kuifanya idadi ya wanajeshi wa Israel walioangamia mwaka jana kufikia 145.

Takwimu za Wizara ya Vita ya Israel zinaonyesha pia kuwa, walowezi 56 wa Kizayuni waliangamizwa mwaka jana, idadi ambayo ni kubwa kuwahi kuushuhudiwa katika kipindi cha mwaka mmoja tangu mwaka 2018.
Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, idadi ya askari wanaokimbia kuhudumu ndani ya jeshi la utawala haramu wa Kizayuni Israel, imezidi kuongezeka huku suala la matatizo ya kisaikolojia likitajwa kuwa ndio sababu.
Katika miaka ya hivi karibuni kambi ya muqawama huko Palestina imeimarika mno na kutoa pigo kwa utawala ghasibu wa Israel, hali ambayo imewafanya askari wa Israel kuingiwa na kiwewe huku kesi za walowezi wa Kizayuni wanaotaka kukimbia kutoka Israel zikiongezeka.