-
UNIFIL yapinga madai ya Israel kuhusu silaha za Hizbullah
Dec 10, 2025 02:42Kamanda wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) amesema kuwa ujumbe wa kulinda amani wa kimataifa haujapata ushahidi wowote kuhusu Harakati ya Hizbullah kujenga upya uwezo wake wa kijeshi, akikanusha madai ya Israel yaliyotumika kama kisingizio cha kushambulia kusini mwa Lebanon.
-
Israel yalaaniwa vikali kwa kuvamia ofisi za UNRWA Quds Mashariki
Dec 09, 2025 07:33Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limesema kwamba polisi wa Israel walivamia makao yake makuu katika Quds (Jerusalem) Mashariki mapema Jumatatu, hatua ambayo limeitaja kuwa “changamoto mpya kwa sheria za kimataifa.”
-
Ripoti: Wapalestina wasiopungua 110 wamefariki katika magereza ya Israel tangu Ben-Gvir achukue wadhifa
Dec 09, 2025 02:39Ripoti mpya imebainisha kuwa angalau Wapalestina 110 wamepoteza maisha ndani ya magereza ya utawala haramu wa Israel tangu Itamar Ben-Gvir, kinara mwenye misimamo mikali wa chama cha 'Nguvu ya Mayahudi' , ateuliwe kuwa waziri wa 'usalama' mnamo Desemba 2022.
-
Ni kwa kiwango gani hatua ya Israel ya kutumia watu wenye ushawishi inaweza kubadilisha simulizi ya kimataifa?
Dec 09, 2025 02:36Kufuatia kuchukizwa sana kwa walimwengu na utawala wa Kizayuni, hasa baada ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala huo huko Palestina, baraza la mawaziri la utawala huo limetenga bajeti ya takriban dola milioni 750 ili kuboresha taswira yake duniani.
-
Wizara ya Afya ya Gaza: Kina cha maafa ya kibinadamu ya Gaza kinachochewa na uhaba wa dawa
Dec 08, 2025 10:30Wizara ya Afya ya Gaza imetangaza kuwa, ukosefu wa dawa na vifaa vya matibabu huko Gaza unaongeza zaidi maafa ya kibinadamu katika eneo hilo.
-
Netanyahu: Israel haitaondoka katika maeneo ya kusini ya Syria iliyoyavamia
Dec 08, 2025 06:30Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu amesema, jeshi la utawala huo halitaondoka katika maeneo liliyoyavamia na kuyakalia kwa mabavu ya kusini mwa Syria.
-
HAMAS: Tuko tayari kukabidhi silaha kwa utawala wa Wapalestina ikiwa Israel itaondoka kikamilifu Ghaza
Dec 08, 2025 02:34Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, iko tayari kukabidhi silaha zake katika Ukanda wa Ghaza kwa mamlaka ya utawala ya Wapalestina itakayosimamia uendeshaji wa eneo hilo, kwa sharti kwamba uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel ukomeshwe kikamilifu.
-
Qatar yakanusha kuisaidia kifedha HAMAS, yasema mawasiliano yao yalianza miaka 13 nyuma
Dec 08, 2025 02:33Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema mawasiliano baina ya Doha na harakati ya Hamas yalianza miaka 10 hadi 13 iliyopita kwa lengo la kurahisisha juhudi za kusitisha mapigano na kupeleka misaada ya kibinadamu Ghaza.
-
Uhispania: Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni ni kinyume na sheria za kimataifa
Dec 07, 2025 06:50Serikali ya Uhispania imetangaza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na utawala wa Israel katika maeneo ya Wapalestina ni kinyume na sheria za kimataifa.
-
Amnesty International yaonya kuhusiana na hali ya Gaza
Dec 07, 2025 06:49Katibu Mkuu wa Amnesty International sambamba na kueleza wasi wasi wake mkubwa kuhusu hali ya Gaza amesisitiza kuwa: Jamii ya kimataifa imejitenga kuiwajibisha Israel na haiangazii na kuzingatia tena hali ya Gaza.