-
Kamari kubwa ya Israel Ghaza yashindwa vibaya kwa kuangamizwa Abu Shabab
Dec 07, 2025 02:25Kuangamizwa kiongozi wa genge la kigaidi na mamluki wa Israel katika Ukanda wa Ghaza, ni kufeli njama za kijasusi za utawala huo huko Ghaza na ni uthibitisho kwamba njama za kutafuta kundi la kuchukua nafasi ya Hamas ni kamari isiyo na mwisho.
-
Imarati yawalipa magaidi mamilioni ya dola kumuokoa mwanamfalme
Dec 07, 2025 02:23Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) imewalipa magaidi wa al-Qaeda zaidi ya dola milioni 23 kama kikomboleo cha mwanamfalme aliyekuwa ametekwa nyara na magaidi hao huko Mali, magharibi mwa Afrika.
-
Mamluki wa Saudia na Imarati watwangana Hadhramaut Yemen
Dec 07, 2025 02:22Muungano wa Kikabila wa Hadramaut wa vibaraka wa Saudi Arabia umeanzisha mashambulio makali dhidi ya vibaraka wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) ukitangaza kwamba kundi la Imarati limekanyaga makubaliano ya kusitisha vita baina yao na linahusika na mauaji yanayoendelea hivi sasa katika jimbo hilo.
-
Jumuiya ya Wafungwa wa Palestina: Israel ina mpango wa kumuua Marwan Barghouthi
Dec 06, 2025 13:42Kundi la kutetea wafungwa wa Kipalestina, The Palestinian Prisoners’ Society (PPS), limeonya juu ya njama hatari ndani ya magareza ya Israel ya kumuua kiongozi mtajika wa Palestina, Marwan Barghouthi, aliyetekwa nyara huku kukiwa na ripoti za ukandamizaji na kudhalilishwa pakubwa kiongozi huyo wa Palestina.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Lebanon inakabiliwa na uchokozi hatari wa Israel
Dec 06, 2025 13:12Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sheikh Naim Qassem amesema kuwa Lebanon inakabiliwa na uchokozi hatari na wa kujitanua wa Israel ambao unapasa kukabiliwa kwa njia zote.
-
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lapasisha maazimio 5 ya kuunga mkono Palestina
Dec 06, 2025 07:54Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepasisha kwa wingi maazimio matano kwa ajili ya Palestina, ikiwa ni pamoja na kuongeza muda wa shirika la UNRWA, kulaani vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kuunga mkono haki za wakimbizi wa Kipalestina.
-
Nchi za Kiislamu zaonya kuhusu mpango wa Israel wa kuwahamisha kwa nguvu raia wa Gaza
Dec 06, 2025 07:50Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi nane za Kiislamu wameeleza wasi wasi wao mkubwa kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya maafisa wa Israel kuhusiana na kufunguliwa kwa upande mmoja kivuko cha Rafah na kuwahamishia wakaazi wa Gaza nchini Misri.
-
Uvamizi wa kijeshi wa Wazayuni katika Ukingo wa Magharibi unaendelea
Dec 06, 2025 02:42Duru za habari zimeripoti kwamba wanajeshi na walowezi wa Kizayuni wameendelea kuvamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kuchoma moto nyumba za Wapalestina na kushambulia raia wasio na ulinzi.
-
Mwanamfalme wa Saudia: Tishio hasa la Asia Magharibi ni Israel, si Iran
Dec 06, 2025 02:42Turki Al-Faisal, mwanamfalme wa Saudi Arabia ambaye pia ni mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Saudia amesisitiza katika mkutano wa kimataifa huko Abu Dhabi kwamba, kinyume na wanavyodai baadhi ya watu, tishio hasa la eneo hili la Asia Magharibi si Iran bali ni utawala wa Kizayuni ambao ndio unaohatarisha utulivu wa eneo hili lote.
-
Hamas: Mwisho wa Abu Shabab ndio hatima isiyoepukika ya kila msaliti
Dec 05, 2025 10:50Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeonya kwamba mauaji ya mshirika wa Israel na kiongozi wa genge lenye uhusiano na Daesh, Yasser Abu Shabab, ni hatima isiyoepukika ya kila mtu anayechagua kulisaliti taifa na nchi yake na kushirikiana na utawala ghasibu wa Israel.