Umoja wa Mataifa: Mauaji ya Gaza, changamoto kwa ubinadamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i104510-umoja_wa_mataifa_mauaji_ya_gaza_changamoto_kwa_ubinadamu
Akigusia ongezeko la idadi ya mashahidi wanaouawa katika Ukanda wa Ghaza kutokana na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu amesema: Mauaji ya Ghaza yanatoa changamoto kubwa kwa suala zima la ubinadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 08, 2023 04:30 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Mauaji ya Gaza, changamoto kwa ubinadamu

Akigusia ongezeko la idadi ya mashahidi wanaouawa katika Ukanda wa Ghaza kutokana na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kibinadamu amesema: Mauaji ya Ghaza yanatoa changamoto kubwa kwa suala zima la ubinadamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Jumatano asubuhi ya shirika la habari la IRNA, Martin Griffiths, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu, huku akielezea masikitiko yake kuhusu kupita elfu kumi idadi ya mashahidi wa Gaza wa mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza amesema kuwa mauaji hayo ya kimbari ni changamoto kubwa ubindamu.

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema hapo kabla katika taarifa  kwamba Gaza imegeuka kuwa kaburi la watoto, kwa sababu kila siku mamia ya wavulana na wasichana wa Palestina wanauawa au kujeruhiwa katika eneo hilo.

Ukanda wa Ghaza

Ametoa wito wa kusitishwa vita mara moja, kutolewa misaada zaidi kwa ajili ya Ghaza na kulindwa  raia, hospitali, vituo vya Umoja wa Mataifa, makazi ya raia na shule katika eneo hilo.

Katika kukabiliana na zaidi ya miongo saba ya uvamizi na ukandamizaji wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, wanamuqawama wa Palestina walitekeleza operesheni ya kushtukiza ya Kimbunga cha Al-Aqsa kutokea Gaza  tarehe 7 Oktoba, dhidi ya maeneo ya utawala huo unaokaliwa Quds kwa mabavu. Katika kulipiza kisasi na kufidia kushindwa kwake na kusimamisha operesheni za wanamuqwama, utawala wa Isreal umefunga vivuko vyote vya Ukanda wa Ghaza na hadi sasa bado unaendelea kushambulia kinyama eneo hilo kwa mabomu ya kila aina.

Utawala wa Kizayuni bado unendeleza mauaji yake ya kimbari na kinyama huko Ghaza licha ya kuongozeka hasira na wasiwasi wa walimwengu kuhusu ukatili unaofanywa dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Palestina na matakwa mengi ya kukomeshwa vita katika ukanda huo.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Palestina alitangaza Jumanne idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza kuwa ni zaidi ya 10,000.