Washington Post: Marekani imetengwa kwa kuiunga mkono Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i106100-washington_post_marekani_imetengwa_kwa_kuiunga_mkono_israel
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, himaya na uungaji mkono kamili wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeifanya Washington kuwa chini ya mashinikizo ya ndani na nje ya Marekani.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Dec 17, 2023 06:26 UTC
  • Joe Biden
    Joe Biden

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa, himaya na uungaji mkono kamili wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel umeifanya Washington kuwa chini ya mashinikizo ya ndani na nje ya Marekani.

Washington Post limeripoti kuwa, himaya na misaada ya serikali ya Rais Joe Biden kwa hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza umeibua shutuma na ukosoaji mkubwa dhidi ya serikali ya nchi hiyo ndani na nje ya Marekani.

Maafisa kadhaa wa Marekani, ambao hawakutaka majina yao yatajwe, wameliambia gazeti la Washington Post kwamba: "Wakati mwingine gharama za kidiplomasia haziwi wazi na dhahiri. Tunataka nchi mbalimbali ziwe na mtazamo chanya kuhusu Marekani na ziwe na hamu ya kutuunga mkono na kushirikiana nasi. Lakini wakati mawazo ya umma katika nchi nyingi yanapoipa Marekani kisogo, kazi yetu huwa ngumu kupata uungwa mkono na umma."

Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani amesema: Utawala wa Biden umekuwa ukijivunia kurejesha uhusiano wa Marekani duniani kote, lakini sasa imetengwa katika eneo la Asia Magharibi na duniani, jambo ambalo sio zuri.

Katika matamshi ambayo hajawahi kuyatoa hapo awali, hivi karibuni Joe Biden alilazimika kuutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kwamba kutokana na jinai na ukatili mwingi uliofanya, umezifanya nchi za dunia zishindwe kuuunga mkono utawala huo. 

Washington Post limeripoti kuwa, mfano dhahiri zaidi wa kutengwa Marekani duniani umeonekana katika vikao vya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa ambako imekuwa ikitumia kura ya veto peke yake kuukingia kifua na kuuhami utawala haramu wa Israel dhidi ya maamuzi ya aghlabu ya nchi zote duniani.