Jul 01, 2024 05:49 UTC
  • Chama cha Macron chapigwa mweleka katika uchaguzi wa Bunge Ufaransa

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa imetangaza matokeo ya awali ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge nchini humo ambapo chama cha "French National Communist Party" kimepata viti vingi na kuushinda muungano wa vyama unaoongozwa na rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron.

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge wa nchi hiyo imevichuanisha vyama vitatu ambavyo ni kile cha siasa kali za mrengo wa kulia cha "French National Communist Party" kinachoongozwa na Le Pen na Jordan Bardela, muungano wa vyama vyenye msimamo wa wastani unaoongozwa na Macron uitwao " Pamoja kwa ajili ya Jamhuri" na muungano wa "New Popular Front", ambao una vyama vya kushoto na vyama vya kijani. Matokeo ya awali ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge wa Ufaransa, yanaonesha kuwa asilimia 34.2 ya wapiga kura wamekipigia kura chama cha Marine Le Pen.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya awali ya uchaguzi wa bunge yaliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa, chama cha "New Popular Front" kimeshika nafasi ya pili baada ya chama cha Le Pen kwa kupata asilimia 29.1 ya kura. Muungano huo unajumuisha vyama vya LFI, PS, PCF, Radical Party na kile cha kupigania mazingira cha EEVL. Muungano unaoongozwa na Macron umeshindwa vibaya. Umeshika nafasi ya mwisho kwa kupata asilimia 21.5 ya kura licha ya kuweko madarakani kwa miaka mingi. 

Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa wabunge wa Ufaransa ilifanyika jana (Jumapili) na awamu ya pili ya uchaguzi huo wa mapema wa bunge la Ufaransa imepangwa kufanyika Jumapili ijayo ya Julai 7. Uchaguzi wa Bunge la Ulaya ndio uliomlazimisha Rais wa Ufaransa kuitisha uchaguzi wa mapema wa bunge nchini mwake.

Tags