Kan'ani: Uchaguzi wa Venezuela ni dhihirisho la kuimarika mfumo wa demokrasia
(last modified Mon, 29 Jul 2024 12:20:48 GMT )
Jul 29, 2024 12:20 UTC
  • Kan'ani: Uchaguzi wa Venezuela ni dhihirisho la kuimarika mfumo wa demokrasia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameutaja uchaguzi wa rais uliofanyika nchini Venezuela uliokuwa na hamasa kubwa kuwa ni dhihirisho la kuimarika mfumo wa demokrasia

Uchaguzi wa Rais wa Venezuela ulifanyika jana Jumamosi na Nicolas Maduro ameibuka na ushindi kwa kupata asilimia 51.2 ya kura zilizopigwa. 

Nicolas Maduro ameibuka na ushindi katika uchaguzi wa Rais wa Venezuela

Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo ametuma ujumbe katika mtandao wa kijamii wa X akipongeza kufanyika vizuri uchaguzi wa Rais wa Venezuela na ushindi wa Nicolas Maduro, na kuandika kuwa: Kufanyika uchaguzi huo ulioshirikisha idadi kubwa ya wananchi na kusimamiwa na mamia ya waangalizi wa kimataifa kutoka nchi, taasisi na mashirika mbalimbali, ni dhihirisho la kuimarika mfumo wa demokrasia nchini humo.  

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu inatangaza tena uungaji mkono na mshikamano na Jamhuri ya Venezuela kwa ajili ya kusogeza mbele  mipango ya maendeleo ya kitaifa na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili. 

Tags