Da Silva: Tutalipiza kisasi dhidi ya ushuru wa Trump
-
Luiz Inacio Lula da Silva
Rais wa Brazil ametangaza kuwa: "Iwapo Donald Trump atatoza ushuru kwa bidhaa za Brazil, tutachukua hatua sawa za kulipizia kisasi."
Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba: "Suala hili ni rahisi sana. Iwapo Donald Trump ataweka ushuru kwa bidhaa za Brazil, tutachukua hatua mfano wake."
Rais wa Marekani, Donald Trump, hivi majuzi aliitaja Brazili kuwa miongoni mwa nchi anazoamini kuwa "zina madhara" kwa Marekani, na ziko kwenye orodha ya nchi zitakazozidishiwa ushuru.
Rais Da Silva aliendelea kusema: "Trump ni Rais wa Marekani na mimi ni Rais wa Brazil. Ninaiheshimu Marekani na nataka Trump aiheshimu Brazil."
Inafaa kukumbusha kuwa Marekani ni mnunuzi mkuu wa mafuta, bidhaa za chuma, kahawa, ndege na juisi ya machungwa kutoka Brazili, na mkabala wake, nchi hiyo ya Amerika Kusini hununua bidhaa za nishati, dawa, vipori vya ndege na bidhaa nyinginezo kutoka Marekani.