Wall Street Journal: Trump anahaha kutaka kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Iran
Apr 05, 2025 02:35 UTC
Gazeti la Marekani la Wall Street Journal limewanukuu maafisa wa nchi hiyo na kuripoti kuwa, Washington inajaribu kutoa mashinikizo ili iweze kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Iran kuhusiana na kadhia ya nyuklia.
Rripoti ya gazeti hilo imesema, serikali ya Trump inapigania kufikia "lengo la kupatia umaarufu la kuukongoa mpango wa nyuklia wa Tehran".
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya Washington inafanya kila njia ili kupiga hatua kubwa zaidi ya kufikia makubaliano kuliko yale yaliyofikiwa katika zama za utawala wa Obama ya JCPOA na kufanikisha kulifikia lengo hilo ndani ya kipindi cha muda mfupi zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti kadhaa, Rais wa Marekani amedai kuwa Tehran inataka kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Washington.
Madai hayo ya Trump yanatolewa katika hali ambayo, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyidd Abbas Araghchi alipozungumza siku ya Ijumaa, Machi 28, kando ya maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, alifuta uwezekano wa kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani, lakini akasema, mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yalishakuwepo tokea huko nyuma, na kwamba hivi sasa pia kama itahitajika, yanaweza kufanyika.
Kabla ya hapo, tovuti ya habari ya Axios iliwanukuu maafisa wa Marekani na kuripoti kuwa, baada ya kupokea jibu la barua iliyoipelekea Iran, serikali ya Trump imeshughulika mno kuchunguza kwa uzito mkubwa pendekezo la Iran la kufanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja juu ya kadhia ya nyuklia.../
Tags