Foreign Policy: Operesheni za kijeshi za Marekani dhidi ya Yemen zimegonga mwamba
Apr 24, 2025 04:13 UTC
Jarida la Foreign Policy la nchini Marekani limeandika kuwa operesheni za kijeshi za Marekani dhidi ya Yemen zimefeli na kugonga mwamba.
Jarida hilo limeashiria mashambulizi yasiyo na tija ya Marekani dhidi ya ngome za Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen, Sera za Kigeni na kuandika kuwa, wiki tano baada ya serikali ya Donald Trump kuanzisha mashambulizi yake dhidi ya Yemen, yameibuka matatizo makubwa kadhaa ambayo yanaonyesha kuwa rais wa Marekani atakuwa na kibarua kigumu cha kuzifanya bwabaja zake ziakisi natija halisi.
Kwa mujibu wa Foreign Policy, operesheni za mashambulizi ya kijeshi za Marekani dhidi ya Yemen hadi sasa zimeshindwa kufikia malengo yake yaliyotangazwa, yaani kuwezesha vyombo vya usafiri wa majini kufanya safari zao tena kwa uhuru katika Bahari Nyekundu na kuzuia kufanywa hujuma za mashambulio dhidi ya vyombo hivyo.
Ripoti ya jarida hilo mashuhuri la nchini Marekani inaeleza kwamba, safari za vyombo vya majini kupitia Bahari Nyekundu na Mfereji wa Suez zingali ni chache mno kutokana na mashambulizi ambayo hadi sasa yameshaigharimu Marekani zaidi ya dola bilioni moja.
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen navyo pia vimeonya juu ya vilichokiita kutumbukia na kunasaTrump kwenye "kinamasi" cha Yemen sambamba na kushadidisha mashambulizi yao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na manowari za Marekani katika eneo hilo.../