Makamu wa Rais wa Marekani aishambulia Ujerumani, asema "imejenga upya Ukuta wa Berlin"
Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance amelinganisha jinsi serikali ya Ujerumani inavyoamiliana na chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany (AfD) kuwa ni sawa na kujenga upya Ukuta wa Berlin.
"Magharibi kwa pamoja iliubomoa Ukuta wa Berlin. Na sasa umejengwa upya - na si na Wasovieti au Warusi - , bali na serikali ya Ujerumani", ameongezea kueleza Vance.
Kiongozi mwenza wa chama hicho cha mrengo wa kulia nchini Ujerumani, Alice Weidel, ameituhumu serikali kuwa inajaribu kuzima upinzani.
Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa X, Weidel amesema: "kwa vile AfD ndicho chama chenye nguvu zaidi katika uchaguzi sasa, wanataka kukandamiza upinzani na uhuru wa kujieleza" .
AfD ilianzishwa mwaka 2013 na ilishka nafasi ya pili katika uchaguzi wa shirikisho uliofanyika mwezi Februari kwa kunyakua viti 152 katika bunge la Ujerumani Bundestag lenye viti 630.../