FIFA yatakiwa kuifukuza Israel katika jumuiya hiyo, imeuwa wanasoka 439
Kampeni maalumu imeanzishwa dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ikitaka kusimamishwa uanachama wa Israel kutokana na mauaji ya utawala huo dhidi ya wanamichezo wa Iran na Palestina.
Ripoti zinasema kuwa kampeni ya "Onyesha Israel Kadi Nyekundu" ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hatimaye imeigeukia FIFA, ikitaka shirikisho hilo la mpira wa miguu lishinikizwe ili kusimamisha uanachama wa utawala haramu wa Israel.
Israel imewauwa wanasoka 439 tangu kuanza kwa vita dhidi ya Gaza katika kipindi cha miezi 21 iliyopita.
Utawala huo pia umewaua shahidi wanamichezo 43 wa fani mbalimbali katika vita vya siku 12 dhidi ya Iran.
Kampeni hiyo ya kimataifa dhidi ya Israel ilianza miezi 4 iliyopita katika viwanja vya soka na hadi sasa imefanywa katika nchi 26 tofauti na watazamaji kutoka zaidi ya vilabu 80 vya michezo.
Kampeni hiyo inapanga kuchapisha picha katika akaunti rasmi za FIFA mtandaoni yenye maudhui "Ionyeshe Israel Kadi Nyekundu Sasa."

Mauaji ya wanasoka na wanariadha na uharibifu wa asilimia 90 ya miundombinu ya michezo ya Ukanda wa Gaza ni ukiukwaji wa wazi wa sheria za FIFA, na kwa mujibu wa sheria za jumuiya hiyo, shirikisho la soka la Israel linapaswa kusimamishwa.