Russia: Kurutubisha Iran urani kwa 60% ni mjibizo kwa vikwazo ilivyowekewa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128084-russia_kurutubisha_iran_urani_kwa_60_ni_mjibizo_kwa_vikwazo_ilivyowekewa
Mwakilishi wa Russia katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao mjini Vienna amesema, hatua ya Iran kurutubisha madini ya urani hadi kiwango cha asilimia 60 ni mjibizo kwa vikwazo na mashinikizo ya kimataifa inayowekewa.
(last modified 2025-07-08T14:09:57+00:00 )
Jul 08, 2025 14:06 UTC
  • Russia: Kurutubisha Iran urani kwa 60% ni mjibizo kwa vikwazo ilivyowekewa

Mwakilishi wa Russia katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao mjini Vienna amesema, hatua ya Iran kurutubisha madini ya urani hadi kiwango cha asilimia 60 ni mjibizo kwa vikwazo na mashinikizo ya kimataifa inayowekewa.

Iran imerutubisha madini ya uranium hadi kiwango cha asilimia 60 katika hali ambayo mazungumzo ya nyuklia yamefikia kwenye mkwamo na vikwazo vya kidhalimu vya kiuchumi ilivyowekewa Tehran vingali vinaendelea.

Ulyanov amesisitiza kuwa, hatua hiyo ya Iran imezitia wasiwasi mkubwa nchi zinazoiwekea mashinikizo Tehran.

Kwa mtazamo wa wachambuzi wa mambo pia, hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kurutubisha urani hadi kiwango cha asilimia 60 imechukuliwa kwa lengo la kutoa jibu kwa mashinikizo ya madola ya Mag haribi yakiongozwa na Marekani na imeibua wasiwasi mpya kwa nchi hizo.

Wachambuzi hao wanaamini kuwa, hatua hiyo itakuwa na taathira kwa mazungumzo ya nyuklia na uhusiano wa kimataifa.

Hali hiyo inaakisi changamoto tata zitakazoibuka katika diplomasia ya nyuklia na haja ya kutafuta suluhisho endelevu na la kudumu ili kupunguza mivutano na kurudi kwenye mazungumzo chanya na yenye kujenga.../