Ripota Maalumu wa UN aihimiza EU isimamishe ushirika wake na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128386
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, Francesca Albanese, ameuhimiza Umoja wa Ulaya usitishe makubaliano ya ushirikiano na utawala wa kizayuni wa Israel, akisema EU ina wajibu wa kisheria wa kutekeleza sheria za kimataifa.
(last modified 2025-07-16T08:01:47+00:00 )
Jul 16, 2025 07:53 UTC
  • Ripota Maalumu wa UN aihimiza EU isimamishe ushirika wake na Israel

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, Francesca Albanese, ameuhimiza Umoja wa Ulaya usitishe makubaliano ya ushirikiano na utawala wa kizayuni wa Israel, akisema EU ina wajibu wa kisheria wa kutekeleza sheria za kimataifa.

Wakati mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana makao makuu ya umoja huo mjini Brussels kujadili hali ya Mkataba wa Ushirika kati ya umoja huo na Israel, pamoja na mambo mengine, Albanese ametuma jumbe kadhaa kwenye mtandao wa X za kuitaka EU ichukue hatua kulingana na maamuzi ya taasisi za kimataifa.

Mkutano wa “kihistoria,” ameandika ripota huyo maalumu wa UN “ingepasa uwe mkutano utakaopelekea kuhitimishwa mauaji ya kimbari, kusambaratishwa ukaliaji ardhi wa ‘milele’ unaofanywa na Israel na ubaguzi wa rangi wa apathaidi, na mwanzo wa kupatikana haki na uwajibikaji.”

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Brussels ili kupima hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya Israel kufuatia mapitio ya makubaliano kati ya jumuiya hiyo na utawala huo wa kizayuni yaliyozinduliwa mwezi Mei baada ya wito kutoka kwa nchi wanachama na mashirika ya kiraia.

Japokuwa kusimamishwa kikamilifu makubaliano hayo kunahitaji kupitishwa kwa kauli moja, kusimamishwa kwa baadhi ya vipengee kama vile biashara, utafiti au mazungumzo ya kisiasa kunawezekana kwa wingi wa kura.

Uhispania, Ireland na Slovenia zimeunga mkono kusimamishwa makubaliano hayo wakati nchi nyingine, zikiwemo Ujerumani, Austria, Czechia na Hungary zinapinga…/