Thailand na Cambodia zasitishaji mapigano 'bila masharti'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128874-thailand_na_cambodia_zasitishaji_mapigano_'bila_masharti'
Thailand na Cambodia zimekubaliana kusitisha mapigano "bila masharti" kuanzia jana Jumatatu usiku wa manane.
(last modified 2025-07-28T23:02:59+00:00 )
Jul 28, 2025 23:02 UTC
  • Thailand na Cambodia zasitishaji mapigano 'bila masharti'

Thailand na Cambodia zimekubaliana kusitisha mapigano "bila masharti" kuanzia jana Jumatatu usiku wa manane.

Tangazo hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim, kufuatia mazungumzo yaliyofanyika nchini Malaysia, nchi ambayo kwa sasa inaongoza Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN).

Taarifa zinasema kuwa, viongozi wa Thailand na Cambodia walikubaliana siku ya Jumatatu, Julai 28, kusitisha mapigano "mara moja na bila masharti" ili kumaliza mapigano mabaya ambayo yamezuka katika siku za hivi karibuni kwenye mpaka wao wa pamoja.

Usitishaji huu wa mapigano umeanza kutekelezwa "saa sita usiku wa kuamkia leo. Ni makubaliano ya kudumu," ametangaza Ibrahim akiwa pamoja na mawaziri wakuu wa Cambodia na Thailand. Hii ni hatua muhimu ya kwanza ya kurejesha amani na usalama."

Mvutano kati ya majirani hao wawili wa Kusini-Mashariki mwa Asia uliibuka tena mwishoni mwa mwezi Mei baada ya kifo cha mwanajeshi wa Cambodia wakati wa mapigano makali kwenye mpaka. Tangu wakati huo, majeshi yote mawili yameongeza sana uwepo wao katika eneo hilo, na kuzidisha mzozo ambao tayari ulikuwa na wasiwasi, haswa kwa muungano dhaifu wa serikali ya Thailand.

Mapigano yalianza tena siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita, na muda wa siku nne tu yalikuwa mapigano mabaya zaidi ya ghasia kati ya nchi hizo mbili katika kipindi cha miaka 13. Mapigano hayo yamesababisha vifo vya takriban watu 36 na kusababisha kuhamishwa kwa zaidi ya watu 200,000 wanaoishi karibu na mpaka. Kila upande umemtuhumu mwenzake kwa kuanzisha mapigano hayo.