Baada ya hofu kuongezeka; wafanyakazi wa ubalozi wa Israel Ugiriki waondolewa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129260-baada_ya_hofu_kuongezeka_wafanyakazi_wa_ubalozi_wa_israel_ugiriki_waondolewa
Baada ya kuhamishwa wafanyakazi wa ubalozi wa Israel katika Umoja wa Falme za Kiarabu, safari hii duru za Israel zinaripoti kuondolewa kwa wafanyakazi ubalozi wa utawala huo mjini Athens, mji mkuu wa Ugiriki.
(last modified 2025-08-07T08:27:51+00:00 )
Aug 07, 2025 08:27 UTC
  • Baada ya hofu kuongezeka; wafanyakazi wa ubalozi wa Israel Ugiriki waondolewa

Baada ya kuhamishwa wafanyakazi wa ubalozi wa Israel katika Umoja wa Falme za Kiarabu, safari hii duru za Israel zinaripoti kuondolewa kwa wafanyakazi ubalozi wa utawala huo mjini Athens, mji mkuu wa Ugiriki.

Kanali ya Televisheni ya Al-Masirah ya Yemen ikilinukuu gazeti la Kizayuni la "Israel Hayom" imeripoti kuwa, kufuatia kuongezeka mivutano na chuki dhidi ya Wazayuni huko Ugiriki, wafanyakazi wa ubalozi wa Israel mjini Athens wameondolewa katika makaazi yao.

 Uamuzi wa kuondolewa wafakanyakazi hao wa ubalozi wa Israel umechukuliwa kutokana na vitisho na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa raia wa Israel katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens.

Maafisa wa Tel Aviv bado hawajatoa radianali yoyote kuhusiana na habari hii. Hivi majuzi Kituo cha Televisheni cha Israel cha Channel 12 pia kilitangaza mnamo kwamba Israel ilikuwa imezihamisha timu zake zote za kidiplomasia na kiutawala kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Hatua hii ilijumuisha wafanyakazi kutoka misheni rasmi, ikiwa ni pamoja na wajumbe wa kidini. Ripoti hiyo imeongeza kuwa sababu ya kuhamishwa huko ni maonyo ya uwezekano wa operesheni dhidi ya raia wa utawala wa kizayuni Israel katika nchi ya Imarati. Hayo yanajiri katika hali ambayo, Uholanzi imewataja mawaziri wa Israeli Itamar Ben-Gvir na Bezalel Smotrich kuwa watu wasiokubalika na hivyo imewapiga marufuku kuingia nchini humo kutokana na vitendo vyao vya kuwachochea walowezi wa Kizayuni kuendesha ghasia na vitendo vya mabavu dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na maangamizi ya kizazi katika Ukanda wa Gaza.