Korea Kaskazini yaionya Korea Kusini kuhusu vitendo vya 'uchochezi'
Korea Kaskazini imemuonya jirani yake Korea Kusini kuhusu vitendo vya 'uchochezi' na kumtaka aachane na hatua hizo kwani zitakuwa na matokeo mabaya.
Korea Kaskazini imeelezea ufyatuaji wa risasi za onyo na jeshi la Korea Kusini kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili kama "uchochezi wa makusudi" na kuionya Seoul kwamba kurudia vitendo kama hivyo kutakabiliwa na mashambulizi makubwa.
Mvutano kwenye Peninsula ya Korea umeongezeka tena huku mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Seoul na Washington yakiendelea. Korea Kaskazini imetangaza kuwa, jeshi la Korea Kusini lilifyatua risasi za onyo katika eneo la mpaka kati ya nchi hizo mbili siku ya Jumanne (Agosti 18), ambayo inachukuliwa kuwa kitendo cha makusudi cha uchochezi.
Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini viliripoti kwamba jeshi la Korea Kusini limekuwa likiongeza matumizi ya maonyo ya sauti katika maeneo ya mpaka, Reuters iliripoti. Kuanzia mwaka jana (2024) Korea Kaskazini imekuwa ikijenga vizuizi kwenye mpaka wake kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi ya kijeshi na Korea Kusini.
Vyombo vya habari rasmi vya Korea Kaskazini viliripoti kwamba ikiwa maonyo yaliyotolewa katika eneo la mpaka yatapuuzwa katika siku zijazo, Korea Kaskazini itachukua "hatua sawia" dhidi ya kizuizi chochote cha mradi wa ujenzi wa kizuizi na "haitabeba jukumu lolote kwa madhara makubwa yatakayotokea.
Kwa upande wake jeshi la Korea Kusini limetangaza katika taarifa: "Mnamo Jumanne (Agosti 19), idadi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini waliokuwa wakifanya kazi katika eneo la mpakani walivuka "mstari wa mipaka wa kijeshi" kati ya nchi hizo mbili, na jeshi la Korea Kusini lilifyatua risasi za onyo, na kisha vikosi vya Korea Kaskazini vilirejea kaskazini mwa mstari huo.