Russia yatungua droni ya Ukraine iliyokusudia kushambulia kinu cha nyuklia cha Kursk
https://parstoday.ir/sw/news/world-i129928-russia_yatungua_droni_ya_ukraine_iliyokusudia_kushambulia_kinu_cha_nyuklia_cha_kursk
Vikosi vya ulinzi wa anga vya Russia vimeitungua ndege isiyo na rubani ya Ukraine (Droni) iliyokuwa imekusudia kutekeleza shambulizi katika kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Kursk cha Russia (KNPP).
(last modified 2025-10-16T03:06:03+00:00 )
Aug 24, 2025 10:53 UTC
  • Russia yatungua droni ya Ukraine iliyokusudia kushambulia kinu cha nyuklia cha Kursk

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Russia vimeitungua ndege isiyo na rubani ya Ukraine (Droni) iliyokuwa imekusudia kutekeleza shambulizi katika kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Kursk cha Russia (KNPP).

Droni hiyo imetunguliwa karibu na kinu hicho cha nguvu za nyuklia cha Russia. 

Ripoti zinasema kuwa, baada ya droni hiyo ya Ukraine kuanguka ililipuka na kusababisha madhara kwa transofoma karibu na eneo hilo. 

Taarifa kutoka kinu cha nguvu za nyuklia cha Kursk imeeleza kuwa hivi sasa, kitengo cha tatu cha nguvu za nyuklia kinafanya kazi katika kinu hicho huku kitengo cha nne kikifanyiwa matengenezo.  

Kutunguliwa kwa ndege hiyo isiyo na rubani ya Ukraine karibu na kinu cha nguvu za nyuklia cha Russia kumesababisha kuwaka moto na hivyo kupelekea kupungua nguvu ya uzalishaji umeme. Uzalishaji wa Kitengo cha tatu cha mtambo wa kuzalisha umeme umepunguza kwa asilimilia 50 kufuatia hujuma hiyo ya Ukraine. 

Wiki iliyopita pia, jeshi la Ukraine lilitekeleza shambulizi katika bomba la Russia linalosafirisha mafuta kuelekea Ulaya ya Kati.