Mwandishi wa Uingereza: Vyombo vya habari vya Magharibi vinapotosha ukweli wa mambo kuhusu njaa huko Gaza
Mwandishi mmoja wa Kiingereza amekiri kwamba vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vinaathiriwa na ushawishi wa utawala katili wa Israei katika kuripoti jinai za utawala huo dhidi ya watu wa Palestina.
Katika kuandika habari za mgogoro wa Gaza, vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa vikishutumiwa mara kwa mara kwa kupotosha matukio na kuchapisha upya simulizi chini ya ushawishi wa utawala wa Kizayuni. Mifano wa wazi kuhusu suala hilo ni pamoja na kubadilisha maelezo mafupi ya picha za watoto wenye njaa au kuhusisha vifo vya waathiriwa wa njaa na matatizo ya kiafya yaliyokuwepo tangu huko nyuma.
Aina hii ya utangazaji wa habari sio tu kwamba inapunguza ukweli wa maafa ya kibinadamu huko Gaza, bali pia inaandaa mazingira ya kukanusha utumiwaji njaa kama silaha na kuficha jinai za utawala wa Israel huko Gaza. Rebecca Ruth Gould, mwandishi wa Uingereza amekiri kwamba vyombo vya habari vya Magharibi vinaathiriwa na jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina. Amesema mzingiro wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza ni mfano wa wazi wa mizingiro iliyokuwa ikiwekwa katika enzi za kati.
Kulingana na mwandishi huyu wa Uingereza, vyombo vya habari vya Marekani na Ulaya vinataka kupotosha ukweli wa mambo kwa kuchapisha upya simulizi na kukanusha ukweli wa matukio yanayotokea huko Gaza.