Maelfu waandamana London kupinga ziara ya Trump nchini Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i130934-maelfu_waandamana_london_kupinga_ziara_ya_trump_nchini_uingereza
Maelfu ya wakazi wa jiji la London wameandamana kupinga ziara ya kiserikali ya Rais Donald Trump wa Marekani nchini Uingereza na kumtaja kama kiongozi mbaguzi na mpenda mabavu. Wafanya maandamano wamelaani pia sera za nje za Marekani kuhusu Iran na Gaza.
(last modified 2025-09-18T09:22:23+00:00 )
Sep 18, 2025 07:22 UTC
  • Maelfu waandamana London kupinga ziara ya Trump nchini Uingereza

Maelfu ya wakazi wa jiji la London wameandamana kupinga ziara ya kiserikali ya Rais Donald Trump wa Marekani nchini Uingereza na kumtaja kama kiongozi mbaguzi na mpenda mabavu. Wafanya maandamano wamelaani pia sera za nje za Marekani kuhusu Iran na Gaza.

Baadhi ya waandamanaji waliokuwa wamebeba bendera za Iran, wamelaani mashambulizi ya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii na vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Tehran.

Makundi yanayopinga vita pia yalikuwa yamebeba bendera za Palestina kulaani uungaji mkono na himaya ya  Marekani kwa utawala wa Israel kufuatia vita na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala huo haramu dhidi ya wakazi wa Gaza.

Maandamano hayo yalianza mbele yashirika la utangazaji la BBC na kuendelea kuelekea viwanja vya Bunge la Uingereza. Nayo polisi ya London ilisambaza askari zaidi ya 1,600 ili kudumisha usalama.

Hii ni ziara ya pili ya kiserikali ya Trump nchini Uingereza, ambayo, sawa na ziara yake ya kwanza aliyofanya mwaka 2019, imeambatana na maandamano makubwa dhidi yake.