Trump asaini dikri dhidi ya Ikhwanul Muslimeen
Kwa kutia saini amri ya utendaji dhidi ya Ikhwanul Muslimeen au kwa jina jingine Muslim Brotherhood, Rais Donald Trump wa Marekani ameweka baadhi ya matawi ya kundi hilo la Kiislamu katika orodha ya "mashirika ya kigeni ya kigaidi".
Trump alitangaza Jumatatu kwamba, ametumia madaraka yake kama rais na kwa kuzingatia Katiba na sheria za Marekani, kutia saini amri hiyo ambayo itaruhusu kuchukuliwa baadhi ya matawi au makundi madogo ya Ikhwanul Muslimeen kama mashirika ya kigeni ya kigaidi na pia magaidi maalum wa kimataifa.
Kwa kutia saini amri hiyo ya utendaji, Trump amewaagiza mawaziri wake wa mambo ya nje na fedha kuripoti iwapo baadhi ya matawi ya Ikhwanul Muslimeen, yakiwemo ya Lebanon, Misri na Jordan, yanapasa kuchukuliwa kama mashirika ya kigeni ya kigaidi au la. Amri hiyo pia inaagiza mawaziri kuchukua hatua ndani ya siku 45 baada ya ripoti hiyo kutolewa.
Hatua hiyo kwa mara nyingine tena inaakisi wazi chuki aliyonayo Trump dhidi ya Uislamu na jamii ya Waislamu. Itakumbukwa kuwa rais huyo tayari ametia saini sheria ya kutoingia nchini Marekani raia wa baadhi ya nchi za Kiislamu, kwa visingizio visivyo na msingi.