Vifaa vya tiiba vya Iran sasa kuzalishwa nchini Venezuela
https://parstoday.ir/sw/news/world-i134318-vifaa_vya_tiiba_vya_iran_sasa_kuzalishwa_nchini_venezuela
Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya Venezuela imetangaza kusainiwa makubaliano ya kimkakati na kampuni ya Iran kwa ajili ya kuzindua njia nne za uzalishaji wa vifaa muhimu vya matibabu nchini Venezuela.
(last modified 2026-02-05T12:50:29+00:00 )
Dec 15, 2025 03:06 UTC
  • Dawa za Iran sasa kuzalishwa nchini Venezuela
    Dawa za Iran sasa kuzalishwa nchini Venezuela

Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya Venezuela imetangaza kusainiwa makubaliano ya kimkakati na kampuni ya Iran kwa ajili ya kuzindua njia nne za uzalishaji wa vifaa muhimu vya matibabu nchini Venezuela.

Kuzinduliwa kwa uzalishaji wa vifaa vya matibabu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Venezuela, ambako kunalenga kuhamisha teknolojia na kuvunja ukiritimba wa Magharibi, kunatekelezwa ndani ya fremu ya makubaliano ya miaka 20 kati ya nchi hizo mbili na kujibu mashinikizo ya vikwazo vya Marekani.

Wizara ya Nguvu ya Watu kwa ajili ya Sayansi na Teknolojia ya Venezuela (Mincyt) ilitangaza rasmi kuwa, Kampuni ya Maendeleo ya Kisayansi na Teknolojia ya nchi hiyo imetia saini ushirikiano wa kistratijia na kampuni ya Iran ambayo inajihusisha na masuala ya sayansi.

Akitangaza habari hiyo, Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Venezuela Gabriela Jimenez Ramirez amesisitiza kuwa: Mpango huu ni sehemu ya mafanikio ya mkutano wa 10 wa Kamisheni ya Pamoja ya Ngazi ya Juu kati ya Iran na Venezuela.

Kulingana na Jimenez Ramirez, katika awamu ya kwanza ya makubaliano haya, njia nne za uzalishaji zitawekwa nchini Venezuela ili kutengeneza vifaa muhimu, ikiwa ni pamoja na vichunguzi vya moyo, vichunguzi vya ishara muhimu, na mashine za kupumulia.

Jimenez Ramirez alisema: "Lengo la ushirikiano huu ni kugawana rasilimali na ujuzi wa kiufundi ili kupunguza gharama na kufungua masoko mapya ya kitaifa na kikanda yenye bidhaa bora na za ushindani.