UN yatadharisha kuhusu uhaba wa chakula Yemen
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umetahadharisha kuhusu kushtadi tatizo la njaa na uhaba wa chakula huko Yemen.
Muhammad Hadi Mkurugenzi Mkuu wa WFP katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika amesema kuwa kuendelea tatizo la njaa na uhaba wa chakula huko Yemen na pia kushindwa raia wa nchi hiyo kufikiwa na misaada ya chakuka, kutawaathiri pakubwa raia wa nchi hiyo. Muhammad Hadi amebainisha kuwa, wanawake na watoto wa Yemen ni wahanga wakuu wa mgogoro unaoikabili nchi hiyo na kwamba kwa mujibu wa tathmini zilizofanywa mwezi Juni mwaka khuu, hadi kufikia sasa raia wa Yemen zaidi ya milioni 14 wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula. Amesema watu milioni saba miongoni mwao wana hali mbaya sana huku asilimia 31 ya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano wakikabiliwa na utapiamlo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa Chakula Duniani (WFP) amesisitiza kuwa, taasisi hiyo hivi sasa inatekeleza mradi wa kupambana na utapiamlo kwa watoto elfu wa Yemen walio na umri wa chini ya miaka 5 na pia kuwasasaidia wakina mama wajawazito kwa kuasisi vituo vya tiba 2200.