Dec 03, 2016 13:38 UTC
  • Ban ataka watu wenye ulemavu washirikishwe katika maendeleo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kujumuishwa kikamilifu watu wenye ulemavu katika shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo katika ujumbe wake kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu ambayo imeadhimishwa leo tarehe tatu Disemba

Ban amesema ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu SDGs, inasisitiza  kutoachwa nyuma kwa mtu yeyote na kwamba ili kutimiza hili watu wenye ulemavu wanahitaji kujumuishwa vilivyo katika jamii na maendeleo.

Ametaka mamlaka za kitaifa na serikali za mitaa, zifanya biashara na wadau wote wa kijamii kuimarisha juhudi za kukomesha ubaguzi na kuondoa vikwazo vinavyowazuia watu wenye ulemavu kupata haki zao kisiasa, kiuchumi kijamii na kiutamaduni.

Watu walemavu

Katibu Mkuu ametaka jamii kuhakikisha ushiriki wa kundi hilo na kuzingatia ubinadamu na kutengamana nao. 

Miaka 10 iliyopita, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha mkataba uliosisitiza kuzingatiwa haki za watu wenye ulemavu na kushirikishwa kwao katika maendeleo.

Tags