Fedheha na kashfa za ngono zaendelea kuutikisa utawala haramu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i23380-fedheha_na_kashfa_za_ngono_zaendelea_kuutikisa_utawala_haramu_wa_israel
Msururu wa kashfa na fedheha za ngono unaendelea kuutikisa utawala wa kizayuni wa Isarel na kuzusha maswali mengi kuhusu maadili ya viongozi wa utawala huo baada ya wanawake wengi kujitokeza na kuanika madhila wanayofanyiwa na maafisa wa serikali au katika jeshi la Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 13, 2017 01:21 UTC
  • Fedheha na kashfa za ngono zaendelea kuutikisa utawala haramu wa Israel

Msururu wa kashfa na fedheha za ngono unaendelea kuutikisa utawala wa kizayuni wa Isarel na kuzusha maswali mengi kuhusu maadili ya viongozi wa utawala huo baada ya wanawake wengi kujitokeza na kuanika madhila wanayofanyiwa na maafisa wa serikali au katika jeshi la Israel.

Kesi ya rais wa zamani wa Israel, Moshe Katsav ambaye aliachiwa huru mwezi uliopita baada ya kutumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kuwadhalalilisha wanawake kingono inahesabiwa kuwa mashuhuri zaidi ndani ya utawala haramu wa Israel katika uwanja huo.

Mwaka 2010 rais huyo wa zamani wa Israel alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka wasaidizi wake wawili makhsusi wakati alipokuwa Waziri wa Utalii, kuwadhalilisha kingono na kutoa mlungula kwa mashahidi wa kesi hiyo ili kukwamisha uadilifu.

Askari wa kike wanadhalilishwa katika jeshi la Israel

Katika miezi ya hivi karibuni pia jenerali moja, afisa wa ngazi za juu katika serikali ya Israel na mbunge wa bunge la utawala huo walifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ubakaji na kuwanajisi wanawake.

Mwezi Julai mwaka uliomalizika wa 2016 pia Jenerali Ofek Buchris alijiuzulu katika jeshi la Israel baada ya kupatikana na hatia ya kubaka wanawake. Jenerali huyo wa jeshi la Israel aliweza kukwepa kifungo jela baada ya kufikia makubaliano kutoa fidia na mawakili wa mhanga wake.

Mapatano hayo yamezusha malalamiko mengi ndani ya utawala haramu wa Israel na hasira za raia kuhusu kashfa zinazozidi kuongezeka za ngono na fedheha za ubakaji unaofanywa na maafisa wa ngazi za juu katika serikali na jeshi la utawala huo ghasibu.