Trump: Waueni Waislamu kwa risasi zilizotumbukizwa kwenye damu ya nguruwe
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33296-trump_waueni_waislamu_kwa_risasi_zilizotumbukizwa_kwenye_damu_ya_nguruwe
Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa kutoa kauli za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, Rais Donald Trump wa Marekani ametoa matamshi yanayoashiria kutaka baadhi ya waumini wa Kiislamu kuuawa kwa kutumia risasi zilizotumbukizwa kwenye damu ya nguruwe.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 18, 2017 03:39 UTC
  • Trump: Waueni Waislamu kwa risasi zilizotumbukizwa kwenye damu ya nguruwe

Katika kile kinachoonekana ni muendelezo wa kutoa kauli za chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, Rais Donald Trump wa Marekani ametoa matamshi yanayoashiria kutaka baadhi ya waumini wa Kiislamu kuuawa kwa kutumia risasi zilizotumbukizwa kwenye damu ya nguruwe.

Matamshi ya Trump ni radimali ya shambulizi la kigaidi lililotokea karibu na mji wa Bercelona nchini Uhispania, ambapo watu 13 wanaripotiwa kuuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa. Aidha magaidi watano waliohusika na shambulizi hilo wameuawa.

Masaa machache baada ya tukio hilo ambapo magaidi wametumia mabomu na gari la mizigo kuwagonga wapita njia katika mji wa Cambrils, yapata kilomita 100 kutoka mji wa Bercelona, Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa: Jifunzeni mbinu zilizotumiwa na Jenerali Pershing wa Marekani baada ya magaidi kukamatwa. Hakukuwa na ugaidi wa Kiislamu kwa muda wa miaka 35", mwisho wa munukuu.

Polisi ya Uhispania baada ya hujuma ya Bercelona

Kati ya mwaka (1899–1913), Jenerali John Pershing wa Marekani aliwakandamizi wafungwa Waislamu wa vuguvugu la uasi la Moro nchini Ufilipino na moja ya mbinu alizotumia ni kwa kuwaua wafungwa hao kwa risasi zilizotumbukizwa kwenye damu ya nguruwe. Waasi hao wa Ufilipino walikuwa wakipambana na ubeberu wa Marekani na uwepo wa majeshi yake nchini mwao.  

Hata kabla ya kuingia madarakani, Trump alikuwa anatumia maneno makali yaliyojaa chuki na kejeli dhidi ya Uislamu na Waislamu wakati wa kampeni zake za urais.

Siku chache baada ya kuingia madarakani, bilionea huyo alipasisha agizo la kupiga marufuku kuingia nchini Marekani raia na hata wakimbizi kutoka nchi saba za Kiislamu.