Aug 22, 2017 02:40 UTC
  • Boston Herald: Warepublican wametiwa wasiwasi na hatua za Rais Trump

Gazeti moja linalochapishwa nchini Marekani limeandika katika ripoti yake kuwa wawakilishi wa chama cha Republican wanatiwa wasiwasi na hatua zinazochukuliwa na Rais wa nchi hiyo.

Gazeti la Boston Herald limeandika kuwa, hatua zinazochukuliwa na Rais Donald Trump si tu kuwa zinapingwa na Wademocrat bali zinawatia wasiwasi pia wanachama wenzake katika chama cha Republican.

Gazeti hilo limeendelea kuandika kuwa, kufutwa kazi Steve Bannon mwanastratejia wa ngazi ya juu katika Ikulu ya White House na radiamali ya kushangaza ya Rais wa Marekani mkabala na matukio ya jimbo la Virginia ni miongoni mwa masuala yanayowatia wasiwasi wawakilishi wa chama cha Republican. 

Steve Bannon, mwanastratejia wa ngazi ya juu katika White House aliyefukuzwa na Trump 

Gazeti la Boston Herald limesisitiza kuwa, baadhi ya wawakilishi wa chama cha Republican wametahadharisha kuwa, kutangazwa stratejia mpya ya kijeshi ya Marekani huko Afghanistan ni suala jingine linalowatia wasiwasi.

Ripoti ya gazeti hilo imeweka wazi kwamba, idadi ya wawakilishi wa chama cha Republican ambao hawapo tayari tena kumuunga mkono Rais Trump imeongezeka na kwamba hilo ni tatizo kwa chama hicho.

Tags