Hali ya kifedha ya UN ni mbaya, maafisa 131 kufutwa kazi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i38189-hali_ya_kifedha_ya_un_ni_mbaya_maafisa_131_kufutwa_kazi
Msemaji wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa amesema kuwa hali ya kifedha ya umoja huo ni mbaya hivyo kuna mpango wa kuwafuta kazi maafisa wake 131 kama njia ya kubana matumizi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 27, 2017 23:12 UTC
  • Hali ya kifedha ya UN ni mbaya, maafisa 131 kufutwa kazi

Msemaji wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa amesema kuwa hali ya kifedha ya umoja huo ni mbaya hivyo kuna mpango wa kuwafuta kazi maafisa wake 131 kama njia ya kubana matumizi.

Televisheni ya Russia Today imemnukuu Stéphane Dujarric akisema hayo na kuongeza kuwa, Umoja wa Mataifa umeamua kuwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi wake na kubakisha maafisa 9959 katika makao makuu yake ya mjini New York. 

Kabla ya hapo Nikki Haley, mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alikuwa amesema kuwa, nchi yake ambayo inadhamini sehemu kubwa ya bajeti ya umoja huo, imeamua kutolipa dola milioni 285 ya hisa yake katika bajeti hiyo.

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani

 

Alisema, Umoja wa Mataifa unatumia fedha nyingi sana na hakuna kazi yoyote muhimu unayoifanya.

Hatua hiyo ya Marekani imekuja baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupinga kwa wingi mutlaki wa kura, uamuzi wa Donald Trump wa kuitangaza Quds Tukufu kuwa eti mji mkuu wa utawala pandikizi wa Israel.

Hatua hiyo ya kukataa Umoja wa Mataifa kuburuzwa na Marekani katika suala hilo imeikasirisha Washington na kuamua kupunguza mchango wake inaotakiwa kuulipa kwa ajili ya kuendesha chombo hicho kubwa zaidi ya kimataifa ulimwenguni.