Seneta Graham: Marekani ndiyo inayoulinda utawala wa Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50090-seneta_graham_marekani_ndiyo_inayoulinda_utawala_wa_saudi_arabia
Seneta mashuhuri wa chama cha Republican nchini Marekani amezungumzia udhaifu wa jeshi la Saudi Arabia na kusema kuwa: Marekani ndiyo inayolinda utawala wa kifalme wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 10, 2018 23:07 UTC
  • Seneta Graham: Marekani ndiyo inayoulinda utawala wa Saudi Arabia

Seneta mashuhuri wa chama cha Republican nchini Marekani amezungumzia udhaifu wa jeshi la Saudi Arabia na kusema kuwa: Marekani ndiyo inayolinda utawala wa kifalme wa nchi hiyo.

Seneta Lindsey Graham amekosoa utendaji wa Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Muhammad bin Salman na kusema: Kama si misaada ya Marekani basi Wasaudia wangelazimika kuzungumza lugha ya Kifarsi katika kipindi cha wiki moja tu, na haja ya Marekani kwa Saudi Arabia ni ndogo sana ikilinganishwa na haja ya Saudia kwa Marekani. Lindsey Graham ameyasema hayo akijibu swali la mwandishi wa televisheni ya Fox aliyesema Riyadh ni mshirika mkubwa wa serikali ya Washington katika kukabiliana na Iran.

Akizungumzia mauaji ya mwandishi na mkosoaji wa utawala wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, seneta huyo wa chama cha Rais Donald Trump amesema, Muhammad bin Salman aliyeamuru mauaji ya mkosoaji huyo ni mwendawazimu na mharibifu. Amesema Bin Salman alidhani kwamba, atamburuta mpinzni katika ubalozi wa Saudi Arabia na kumuua kikatili kisha akane mauaji hayo. 

Seta huyo ambayo ni mjumbe katika Kamati ya Jeshi la Marekani kwenye Baraza la Seneti ya nchi hiyo amesema kikao cha Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA na maseneta ndiyo ripoti bora zaidi iliyokwishatolewa hadi sasa kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi na nafasi ya Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia katika mauaji hayo.

Akizungumza kwa kutegemea ripoti hiyo, Lindsey Graham amesema mtu aliyesimamia mauaji ya Khashoggi ni msaidizi mkuu wa Bin Salman na maseneta wote walioshiriki katika kikao hicho wanaamini kwamba, Bin Salman ndiye aliyeamuru mauaji ya Jamal Khashoggi.