Indonesia yaanza kuwatafuta manusura waliofukiwa katika maporomoko ya udongo
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50562-indonesia_yaanza_kuwatafuta_manusura_waliofukiwa_katika_maporomoko_ya_udongo
Timu ya waokoaji imeendelea na zoezi la kutafuta watu ambao bado wako hai baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maporoko ya udongo mashariki mwa Indonesia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 01, 2019 15:04 UTC
  • Indonesia yaanza kuwatafuta manusura waliofukiwa katika maporomoko ya udongo

Timu ya waokoaji imeendelea na zoezi la kutafuta watu ambao bado wako hai baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha maporoko ya udongo mashariki mwa Indonesia.

Maporomoko hayo ya udongo yameuwa watu wasiopungua watano na makumi ya wengine hawajulikani walipo.  

Sutopo Purwo Nugroho msemaji wa Idara Huduma za Waliopatwa na Maafa ya Indonesia leo ameeleza kuwa wafanyakazi wa uokoaji hadi sasa wamepata watu watano walioaga dunia na wanaendelea na zoezi la kuwatafuta watu wengine wasiopungua 38 ambao hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya udongo kutokea katika kijiji kimoja katika mkoa wa Java magharibi mwa nchi hiyo jana Jumatatu. Watu watatu pia wamejeruhiwa katika tukio hilo huku wengine 61 wakihamishiwa katika eneo jingine.

Hata hivyo kuendelea kunyesha mvua, kukatika huduma ya umeme na barabara mbovu yametajwa kuwa masuala yanayokwamisha jitihada za uokoaji katika eneo athirika.

Mafuriko makubwa mkoani Java nchini Indonesia