China yaionya Marekani kuhusu kucheza na moto kwa kuiunga mkonoTaiwan
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53837-china_yaionya_marekani_kuhusu_kucheza_na_moto_kwa_kuiunga_mkonotaiwan
China imesema Marekani ‘inacheza na moto’ kutokana na msururu wa hatua ambazo imezichukua katika Lango Bahari la Taiwan katika kuunga mkono jitihada za kujitenga kikamilifu kisiwa hicho.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
May 31, 2019 23:06 UTC
  • China yaionya Marekani kuhusu kucheza na moto kwa kuiunga mkonoTaiwan

China imesema Marekani ‘inacheza na moto’ kutokana na msururu wa hatua ambazo imezichukua katika Lango Bahari la Taiwan katika kuunga mkono jitihada za kujitenga kikamilifu kisiwa hicho.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wu Qian amesema Marekani imekuwa ikijaribu kutumia Taiwan kuidhibiti China. Amesema hiyo ni ndoto potovu ya Marekani na kuongeza kuwa, hatua ambazo Marekani imezichukua zinaweza kuhatarisha uhusiano wa Beijing na Washington na pia kuhatarisha amani na usalama katika Lango Bahari la Taiwan.

China imetoa tahadhari hiyo baada ya Taiwan kutangaza Alhamisi kuwa inafanya mazoezi ya kijeshi kusini mwa kisiwa hicho.

Meli za kivita katika lango bahari la Taiwan

Kwa muda mrefu sasa China imekuwa ikiituhumu Marekani kuwa hatua zake za kichochezi huko Taiwan zinadhuru mamlaka yake ya kujitawala.

Karibu nchi zote duniani zinaitambua China kama mmiliki wa visiwa vyenye mamlaka ya ndani vya Taiwan. Wakuu wa Beijing wamekuwa wakitekeleza jitihada za kuhakikisha kuwa Taiwan inarejea katika mamlaka kamili ya China baada ya kujitangazia mamlaka ya ndani kufuatia vita vya ndani mwaka 1949.