Amnesty International: Saudi arabia haipasi kumnyonga mfungwa wa kisiasa barobaro
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54009-amnesty_international_saudi_arabia_haipasi_kumnyonga_mfungwa_wa_kisiasa_barobaro
Shirika la Msamaha Dunianii (Amnesty International) limeitaka Saudi Arabia isimnyonge mfungwa wa kisiasa barobaro ambaye alitiwa mbaroni akiwa na miaka 13.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2019 03:05 UTC
  • Amnesty International: Saudi arabia haipasi kumnyonga mfungwa wa kisiasa barobaro

Shirika la Msamaha Dunianii (Amnesty International) limeitaka Saudi Arabia isimnyonge mfungwa wa kisiasa barobaro ambaye alitiwa mbaroni akiwa na miaka 13.

Amnesty International imetangaza kuwa Murtaja Qureiris alitiwa mbaroni mwezi Septemba mwaka 2014 na hivi sasa ana umri wa miaka 18; ambapo Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Saudia ametaka kutekelezwa hukumu ya kifo aliyokatiwa kijana huyo. Shirika hilo la Msamaha Duniani aidha limefichua kuwa Qureiris amekabiliwia na mateso akiwa jela na wakati akihojiwa. Maafisa waliokuwa wakimsaili walimuahidi kijana huyo kuwa wangemuachia huru iwapo angekiri wakosa waliyompachika. 

Murtaja Qureiris akiwa maandamanoni 
 

Mwezi Aprili mwaka huu pia watu 37 walinyongwa siku moja nchini Saudi Arabia na Shirika la Amnesty International lilitangaza kuwa watu wasiopungua watatu miongoni mwa hao walionyongwa walitiwa mbaroni wakiwa na umri wa miaka 16 hadi 17. Vijana hao watatu wote walikuwa Waislamu wa Kishia ambao walikamatwa kwa kosa la kushiriki katika maandamano dhidi ya serikali. Takwimu za Amnesty International zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya hivi karibuni Waislamu wa Kishia zaidi ya 100 wamenyongwa nchini Saudi Arabia kwa sababu za kisiasa.  

Taasisi hiyo ya kimataifa imelaani hukumu hizo za kuwanyonga wananchi wa Saudia na kueleza kuwa hukumu zinazotolewa kwa raia wa nchi hiyo ni za kidhulma.