Indonesia yakadhibisha madai ya kutaka kuanzisha uhusiano na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i65237-indonesia_yakadhibisha_madai_ya_kutaka_kuanzisha_uhusiano_na_israel
Indonesia imekanusha madai ya kipropaganda ya vyombo vya habari vya Wazayuni kwamba inataka kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 17, 2020 04:42 UTC
  • Indonesia yakadhibisha madai ya kutaka kuanzisha uhusiano na Israel

Indonesia imekanusha madai ya kipropaganda ya vyombo vya habari vya Wazayuni kwamba inataka kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.

Teuku Faizasyah, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia amepuuzilia mbali uwezekano wowote wa taifa hilo lenye jamii kubwa zaidi ya Waislamu duniani kuanzisha uhusiano na Israel, na kusisitiza kwamba nchi hiyo haijawahi kufanya mawasiliano yoyote na Tel Aviv.

Amesema nchi hiyo itaendelea kufuata miongozo ya Katiba ikija katika suala Palestina na kwamba sera za kigeni za nchi hiyo ziko wazi kabisa na hazitobadilika.

Msimamo huo uliotolewa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia umekuja baada ya gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post kudai kuwa, baada ya Morocco, Oman na Indonesia zipo mbioni kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel katika wiki zijazo.

Waiondonesia katika maandamano ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa Wapalestina

Wiki iliyopita, Morocco ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na Israel tokea mwezi Agosti wakati mtawala wa Marekani anayeondoka, Donald Trump alipoanzisha mkakati wa kuzishinikiza nchi za Kiarabu kuanzisha uhusiano na utawala huo bandia.

Mbali na Morocco, nchi zingine za Kiarabu ambazo zimeanzisha uhusiano na Israel hivi karibuni ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan ambazo zimeanzisha uhusiano na utawala huo dhalimu katika fremu ya njama za Marekani-Kizayuni za kudhoofisha uungaji mkono wa nchi za Kiarabu kwa harakati za kupigania ukombozi wa Palestina.