Feb 06, 2016 07:58 UTC
  • Zarif aonya dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu Magharibi

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea hofu yake kuhusu kuongezeka kwa visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi dhidi ya Waislamu katika nchi za Magharibi.

Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo mjini London kabla ya kuhitimisha safari yake rasmi ya siku mbili nchini Uingereza na kuongeza kuwa, ni jambo la kusikitisha kuwa nchi za Magharibi zimeifumbia macho kadhia hiyo ya ubaguzi katika misingi ya dini na ukandamizaji, ili kulinda maslahi yao.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekariri kuwa, utawala wa Saudia ndio kikwazo kikuu cha kufikiwa amani na udhabiti katika Mashariki ya Kati huku akisisitiza juu ya utayarifu wa Jamhuri ya Kiislamu wa kushirikiana na nchi zote za eneo kwa ajili ya usalama wa eneo hili.

Zarif ambaye aliondoka London jana usiku kurejea Tehran, alienda kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kuwasaidia Wananchi wa Syria nchini Uingereza.

Akiwa mjini London, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amekutana na kufanya mazungumzo pia na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Tags