Wanazuoni wa Yemen: Kutetea matukufu ya Kiislamu ni wajibu wa kidini
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i134562-wanazuoni_wa_yemen_kutetea_matukufu_ya_kiislamu_ni_wajibu_wa_kidini
Jumuiya ya Maulamaa wa Yemeni ilifanya mkutano mkubwa katika mji mkuu Sanaa siku ya Jumamosi, na kusisitiza jukumu la kidini la wasomi na maulamaa katika kutetea Qur’an na matukufu ya Kiislamu.
(last modified 2026-02-05T12:50:29+00:00 )
Dec 21, 2025 09:44 UTC
  • anazuoni wa Yemen: Kutetea matukufu ya Kiislamu ni wajibu wa kidini
    anazuoni wa Yemen: Kutetea matukufu ya Kiislamu ni wajibu wa kidini

Jumuiya ya Maulamaa wa Yemeni ilifanya mkutano mkubwa katika mji mkuu Sanaa siku ya Jumamosi, na kusisitiza jukumu la kidini la wasomi na maulamaa katika kutetea Qur’an na matukufu ya Kiislamu.

Muungano huo umetoa wito wa kuhamasisha Umma wa  Kiislamu dhidi ya uchokozi wa Marekani na utawala wa Kizayuni, na kuchukua misimamo madhubuti dhidi ya kuidhalilisha Quran Tukufu.

Jumuiya ya Maulamaa wa Yemeni iilifanya mkutano mjini Sanaa chini ya kaulimbiu "Wajibu wa Wasomi katika Kutetea Kitabu cha Mungu na Matukufu na Kuhamasisha Umma kwa Jihad dhidi ya Marekani  na utawala vamizi wa Israel."